Law, crime

Makundi yenye silaha CAR yazidi kutumia watoto jeshjini:UM

Ripoti mpya ya Umoja wa Umoja imeelezea jinsi watoto wanavyoendelea kuingizwa jeshini na makundi yaliyojihami katika Jamhuri ya Afrika ya kati na kutoa wito kwa hatua kuchukuliwa kuzuia vitendo hivyo.

Watu zaidi ya 100 wauawa katika machafuko Syria

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Syria kukomesha mara moja mauaji dhidi ya raia.

Uhalifu wa vita umetekelezwa na serikali na waasi Sri Lanka

Jopo maalumu la wataalamu wa kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuhusu masuala muhimu kwenye mgogoro wa Sri Lanka wamebaini ripoti za uhalifu wa kivita uliotekelezwa na serikali na waasi wa Tamil Tigers.

Wahamaiji zaidi wawasili mjini Benghazi

Meli ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM imewasili kwenye mji wa Benghazi nchini Libya ikiwa na wahamiaji 995 na raia wengine waliojeruhiwa kutoka mji uliokumbwa na mapigano wa Misrata.

Pillay aitaka serikali ya Syria isitishe mauaji dhidi ya waandamanaji

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za binadamu Navi Pillay amesema kuwa njia ambazo serikali ya Syria inazotumia kujibu maandamano hayo hazitakubalika na kuvitaka vikosi vya usalama kukoma kutumia risasi dhidi ya waandamanaji.

Ban azitaka Cambodia na Thailand kusitisha mapigano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anasumbuliwa na ripoti za mapigano mapya yaliyodumu kwa muda wa siku mbili zilizopita kati ya wanajeshi wa Cambodia na Thailand kwenye mpaka kati ya nchi hizo ambapo watu wengi wameuawa.

Ban atao wito wa kutaka kusitishwa ghasia dhidhi ya maandamano ya amani nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu vikali ghasia zinazozidi kuendeshwa dhidi ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani nchini Syria hali ambayo imesababisha kutokea vifo na majeraha mengi na kuutaka utawala wa nchini hiyo kuheshimu sheria za kimataifa na kusitisha umwagaji wa damu.

Tatizo la ubakaji DRC, ni suruba na adha kwa maelfu ya wanawake, ni lazima likomeshwe:UM

Wanawake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hususan Kaskazini Mashariki wanaishi wa hofu kubwa kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ubakaji.

Kuuawa kwa magaidi sio dawa ya ugaidi

Mkutano unaojadili njia za kuzuia na kupambana na ugaidi unaendelea mjini Strasbourg nchini Ufaransa ambapo masuala kadha yanohusu njia za kupambana na ugaidi yanajadiliwa na baraza la ulaya na kamati ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi.

IMO imelaani vikali dhuluma za maharamia wa Somalia

Shirika la umoja wa mataifa linalohusika na usafiri wa majini IMO, limelaani vikali mwenondo unaofanywa na makundi ya kiharamia ambao hutumia mbinu ya kuwateka wasafiri wa habarini kama chambo cha kutimiza matakwa yao.