KJP

Nashukuru FAO badala ya debe 5 za mahindi sasa navuna magunia 30- Mkulima 

Kuelekea mkutano wa Umoja Mataifa kuhusu mifumo endelevu ya vyakula kuanzia shambani hadi mezani, huko mkoani Kigoma nchini Tanzania mradi wa pamoja Kigoma KJP unaoendeshwa kwa pamoja na serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la chakula na kilimo, FAO umezidi kuwajengea kujiamini wakulima kwa kuwa hivi sasa kilimo chao kinahimili mabadiliko ya tabianchi na kiwango cha mavuno kimeongezeka bila uchovu ikilinganishwa na awali.

Muhogo aina ya Mkombozi yawa mkombozi kwa wakulima Kigoma

Nchini Tanzania harakati za Umoja wa Mataifa kujengea uwezo wakulima katika kutambua mbinu bora za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, zimezaa matunda huko mkoani Kigoma baada ya wakulima wa wilayani Kakonko kuvuna zao la muhogo walilopanda kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu
 

Mashine mpya kupunguza muda wa kukamua mawese kutoka saa 8 hadi 2

Umoja wa Mataifa kupitia kituo chake cha biashara, ITC imejibu ombi la wanawake wajasiriamali mkoani Kigoma nchini Tanzania kwa kuwapatia mashine ya kisasa ya kukamua mawese na hivyo kupunguza siyo tu muda wa kukamua mafuta hayo kutoka saa 8 hadi mbili bali pia kupata mafuta yenye ubora zaidi. 

Kilimo hifadhi kinaturejesha ujana – Wanufaika Kigoma

Nchini Tanzania mafunzo ya kilimo hifadhi yaliyotolewa mwaka jana na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa MAtaifa, FAO kwa wakulima mkoani Kigoma yameanza kuzaa  matunda na wakulima ndio mashahidi. 

UNCDF na wadau Tanzania waondolea wakulima hofu ya kupata pembejeo 

Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la mitaji UNCDF na wadau wamezindua mpango wa kutumia teknolojia ya simu ya kiganjani kumwezesha mkulima mkoani Kigoma magharibi mwa taifa hilo kuweza kupata pembejeo za kilimo wakati anapohitaji. 

Wakulima viongozi Kigoma waelimika juu ya kilimo hifadhi 

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa –FAO- nchini Tanzania, chini ya programu ya pamoja ya Kigoma au Kigoma Joint Program, KJP wameendesha mafunzo ya kilimo hifadhi kwa wakulima mkoani Kigoma.

Mashine kutoka ITC yawezesha wanawake Buhigwe kukamua mawese kwa saa 1 badala ya saa 8

Mradi wa pamoja wa Kigoma, KJP nchini Tanzania unaoendeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa umeendelea kuwa baraka kwa wakazi wa mkoa huo ambapo wanufaika wa hivi karibuni zaidi ni kikundi cha wanawake kata ya Janda wilaya ya Buhigwe, kilichopatiwa kiwanda kidogo cha kuchakata mafuta ya mawese, na hivyo kuondokana na njia ya kienyeji.  

Ushirikiano wa Tanzania na UN Kigoma waleta nuru kwa  manusura wa ukatili wa kijinsia

Programu ya pamoja kwa mkoa wa Kigoma, KJP, inayotekelezwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa imeweza kuleta chachu katika mpango wa taifa wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.