Watu 260,000 walioathirika na kimbunga Goni Ufilipino wanahitaji msaada
Mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu wametoa ombi la dola milioni 45.5 ili kuwasaidia watu 260,000 katika maeneo yaliyoathirika zaidi na kimbunga Goni nchini Ufilipino.