Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasaidia harakati za kutoa msaada wa dharura Bahamas nchi ambayo inakabiliwa na athari kubwa zilizosababishwa na kimbunga Dorian, ikiwa ni kimbunga kibaya zaidi kuwahi kukumba visiwa hivyo.
Wakati Umoja wa Mataifa na watoa misaada wengine wakiendelea na shughuli za kutoka msaada katika visiwa vya Bahamas ripoti za hivi punde zinaashiria kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwa mujibu wa Shirika la afya ulimwenguni, WHO.
Kimbunga Dorian kikiendelea kuleta madhara huko visiwa vya Bahamas, ripoti zinasema kwamba watu watano wamethibitishwa kufariki dunia huku mashirika ya Umoja wa Mataif ana wadau wakiwa wamepeleka watendaji wake kufanya tathmini ya uharibifu.