kigoma

22 Januari 2020

Hii leo tunaanza na kauli ya Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa kuhusu changamoto 4 na suluhu 4 kwa ajili ya kuhakikisha mafanikio ya karne ya 21 hayafutiliwi mbali kisha tunakwenda Kigoma kumulika jinsi miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye kilimo inavyoendelea kufuta kilimo cha "tangulia nakuja" husu

Sauti -
13'34"

Kilimo cha “tangulia nakuja” sasa basi Kigoma

Katika mkoa wa Kigoma nchini Tanzania ambako Umoja wa Mataifa unatekeleza mpango wa pamoja kwa ajili ya mkoa huo, (Kigoma Joint Programme) kupitia mashirika yake ikiwemo lile la chakula na kilimo, FAO, matokeo chanya yameanza kudhihirika tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango huo wenye maeneo kadhaa ikiwemo kilimo.

13 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Miaka 10 baada ya tetemeko baya la ardhi nchini Haiti athari zake zinaendelea kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM

Sauti -
11'50"

Mradi wa FAO wawezesha wanafunzi kuwezesha jamii Tanzania

Kutokomeza umasikini uliokithiri ni kitovu cha juhudi za dunia kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na kujenga mustakabali endelevu kwa watu wote lakini mafanikio ya kutomwacha yeyote nyuma hayatapatikana iwapo watu walioachwa nyuma zaidi hawatalengwa kwanza. 

Sauti -
2'

Wafugaji wa nyuki na mafundi seremala Kigoma wapewa mafunzo ili kuboresha mizinga na uzalishaji bora wa asali.

Tarehe 20 ya mwezi huu wa Mei ilikuwa ni siku ya nyuki duniani msisitizo ukiwa katika kutunza wadudu hao wachavushaji wa maua ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa chakula.

Sauti -
5'31"

Mafundi seremala Kigoma wapatiwa mbinu za kutengeneza mizinga bora ya nyuki

Nchini Tanzania mashirika ya Umoja wa Mataifa kupitia mpango wa pamoja wa Kigoma, KJP yamekuwa yakitekeleza miradi mbalimbali ili kusaidia kusongesha maendeleo ya mkoa huo ambao kwa miaka kadhaa umekuwa ukipokea wakimbizi kutoka nchi jirani.

Pamoja na wanawake na watoto wa Tanzania, pia tunawasaidia wakimbizi-WLAC

Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na  asasi mbalimbali za kiaraia, pamoja na serikali wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 kupitia malengo 17 yaani SDGs.

Sauti -
8'24"

08 Februari 2019

Hii leo tunaanzia Tanzania taifa hilo limeshukuriwa kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi na hakikisho ya kwamba katu hawatofurushwa kurejea makwao bali watarejea kwa  hiari na mada kwa kina tunaye Kala Jeremiah, mwanamuziki nguli Tanzania akiangazia masuala ya ukeketaji baada ya kuwepo mkoani Mara k

Sauti -
9'56"

Msaada zaidi kwa Tanzania wahitajika ili ihudumie vyema wakimbizi- Grandi

Kamishna Mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa ,UNHCR, Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Tanzania akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwekeza zaidi mikoa ya kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ambayo ni nyumbani kwa wakimbizi 330,000. 

Miradi ya UN yagusa maisha ya wakulima Tanzania

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo mengine tunaangazia kile ambacho chombo hicho chenye wanachama 193 kinatekeleza kule mashinani ili kuboresha maisha ya wananchi.