Mkoani Kigoma nchini Tanzania, mafunzo yanayotolewa na mashirika ya Umoja wa Matafa likiwemo lile la chakula na kilimo , FAO, mpango wa chakula duniani, WFP na maendeleo ya mitaji, UNCDF kwa wakulima wawezeshaji yamefungua nuru ya mmoja wao na hadi kuwezeshwa na shirika hilo ili aweze kusaidia wakulima wenzake.