Chuja:

Kigoma Joint Programme

FAO Tanzania

Salvation Youth Group wa Kasulu Kigoma Tanzania waushukuru mradi wa KJP 

Mnamo mwaka 2017 mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo FAO, la Mpango wa Chakula Duniani WFP kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la maendeleo ya mitaji UNCDF pia Kituo cha Biashara cha kimataifa ITC, yaliamua kushirikiana kutekeleza mradi wa pamoja Mkoani Kigoma nchini Tanzania, KJP. Kupitia mradi huo unaowahusisha wanawake vijana na wanaume vijana kupitia kwenye vikundi vyao, kikundi cha Salvation Youth Group cha Kasulu Kigoma kimenufaika kwa kupewa mashine ya kutotolesha vifaranga vya kuku kupitia mradi huo.

Sauti
3'21"
FAO Tanzania

FAO imenijengea uwezo wa kufuga nyuki kisasa – Mkulima Kigoma

Mafunzo yaliyotolewa na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO kuhusu mbinu bora za ufugaji nyuki na matumizi ya mizinga bora huko mkoani Kigoma nchini Tanzania, yameanza kuzaa matunda baada ya baadhi ya wafugaji waliopata mafunzo kuchukua hatua na kutekeleza kwa vitendo. Loise Wairimu na ripoti kamili.

Mizinga ya nyuki tayari mtini!  ni katika eneo la Bwana Hijja Katobagula, mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo yaliyoendeshwa mwaka jana wa 2019 wilayani Kibondo kupitia programu ya pamoja ya Kigoma  ya Umoja wa Mataifa, KJP. Mfugaji huyu anasema kuwa

Sauti
2'25"
FAO Tanzania

Mafunzo ya FAO sasa yamewezesha hata waume zetu kufurahia kilimo- Paskazia

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kubadilisha maisha ya wananchi kupitia miradi mbalimbali inayotekeleza huko nchini Tanzania.

Miradi hiyo ni pamoja na ule wa kupatia wakulima mbinu bora za kilimo ili kuongeza kipato, kulinda mazingira, kuepusha ukosefu wa chakula na  kutokomeza umaskini, mradi ambao unatekelezwa na FAO ambalo ni shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, kupitia mradi wa pamoja wa wa Umoja wa Mataifa kwa Kigoma. 

Sauti
4'22"

22 Januari 2020

Hii leo tunaanza na kauli ya Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa kuhusu changamoto 4 na suluhu 4 kwa ajili ya kuhakikisha mafanikio ya karne ya 21 hayafutiliwi mbali kisha tunakwenda Kigoma kumulika jinsi miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye kilimo inavyoendelea kufuta kilimo cha "tangulia nakuja" hususan wilayani Kibondo, tumezungumza na Martine Kapaya.

Sauti
13'34"