Kidal

Walinda amani wa UN kutoka Chad wauawa katika shambulio Mali

Walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa kutoka Chad wameuawa siku ya Jumapili Kaskazini mwa Mali wakati msafara wao ulipokanyaga bomu lililotegwa barabarani karibu na eneo la Aguelhok kwenye jimbo la Kidal.

Guterres alaani shambulizi dhidi ya walinda amani wa MINUSMA Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake hii leo amelaani shambulio dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa lililotekelezwa Timbuktu na Tessalit.

Licha ya purukushani, uchaguzi wafanyika kwa amani Mali

Nchini Mali uchaguzi wa rais umefanyika kwa amani licha ya kuripotiwa kwa visa vya hapa na pale vilivyokwamisha upigaji kura kufanyika katika baadhi ya vituo.