Chuja:

Kaya speaker

UNNewsKiswahili/Assumpta Massoi

Ubunifu wa spika janja Kaya sasa kuanza kuingia sokoni mwakani

Kila uchao Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushiriki wa vijana katika kuleta mabadiliko katika dunia ya sasa na kuhakikisha mustakabali wa kizazi kijacho unakuwa bora. Umoja wa Mataifa ukitoa wito huo vijana nao wanaitikia kuhakikisha kuwa wanatumia stadi zao kubadilisha maisha ya jamii zao kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Miongoni mwa vijana hao ni Isaya Yunge kutoka Tanzania ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni inayotengeneza spika janja, Smart Kaya.

Audio Duration
4'26"