Kaya Maskini

Mradi wa Benki ya Dunia Ghana waleta furaha kwa kaya maskini

Nchini Ghana, Benki ya Dunia inasaidia serikali kuandaa na kutekeleza miradi ya hifadhi ya jamii inayoweza kusaidia taifa hilo la Afrika Magharibi kuimarisha ukuaji wake wa kiuchumi, kupunguza umaskini na kuongeza vipato vya wafanyakazi wa ngazi ya chini na ya kati na hatimaye kuboresha maisha ya wananchi. 

Mradi wa kunusuru kaya maskini mijini huko Ethiopia waondoa unyonge kwa familia 

Nchini Ethiopia mpango wa kusaidia kaya maskini kwa kuzipatia fedha, sasa unaongezwa kiwango cha fedha kutoka dola 13 kwa mwezi hadi dola 21 kwa mwezi baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau kuingia makubaliano ya kusaidia serikali katika mpango huo kwa miezi sita ijayo.

Mpango wa kunusuru kaya maskini Tanzania ni chachu ya kufanikisha SDGs- Tumpe

Katika jitihada za kufanikisha lengo namba moja la malengo 17 ya maendeleo endelevu,SDGs, la kutokomeza umaskini,  Tanzania ilianzisha mfuko wa maendeleo ya jamii uitwao TASAF ukiwa na lengo la kuzinusuru kaya maskini zaidi.