katwa

Eneo la Katwa, Kivu Kaskazini, linaongoza kwa visa vya Ebola-WHO

Shirika la Afya duniani WHO linasema kumekuwepo na ongezeko la wagonjwa wa Ebola kwenye jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC na eneo la Katwa linaongoza kwa maambukizi zaidi. 

Mashauriano ya kijamii DRC yaenda sambamba na harakati dhidi ya Ebola

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hadi kufikia jana ni 679 ikiwa ni ongezeko la vifo 37 tangu siku 5 zilizopita.

Mwitikio wa wananchi kwenye harakati dhidi ya Ebola huko Katwa na Butembo watia moyo- WHO

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema linatiwa matumaini makubwa na harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola huko jimboni Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

MSF na ALIMA wafunga virago Katwa na Butembo, ni baada ya vituo vyao vya kutibu Ebola kushambuliwa

Kufuatia matukio ya kutiwa moto kwa kituo cha kutibu Ebola cha Katwa na kile cha Butembo kushambuliwa na watu wasio na silaha wasiojulikana, vyote jimboni Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeripotiwa hii leo kuwa vituo hivyo viwili sasa havifanyi kazi kabisa.

Sauti -
1'59"

Vituo viwili vya kutibu Ebola Katwa na Butembo vyafungwa, visa vipya 6 vya Ebola vyaripotiwa

Kufuatia matukio ya kutiwa moto kwa kituo cha kutibu Ebola cha Katwa na kile cha Butembo kushambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana, vyote jimboni Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeripotiwa hii leo kuwa vituo hivyo viwili sasa havifanyi kazi kabisa. Shirika la afya ulimwenguni, WHO ambalo limelaani kitendo hicho, sasa linahofu kuwa ugonjwa huo unaweza kusambaa zaidi kutokana na hatua ya baadhi ya mashirika ya kiraia kuondoa wafanyakazi wake kutoka eneo hilo. Martial Papy Mukeba wa Radio  Okapi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO anaripoti zaidi.