Kamishna Mkuu OHCHR

Ubakaji ni kosa lakini kuwahukumu kifo na kuwahasi watekelezaji si suluhu:Bachelet 

Kamishina mkuu wa haki za binadamu amesema ingawa watekelezaji wa ubakaji na mifumo mingine ya ukatili wa kingono lazima wawajibishwe, hukumu ya kifo au utesaji sio jawabu muafaka. 

Kamishna Mkuu Bachelet ataka uchunugzi kuhusu kifo cha Hassan Toufic Dika wa Lebanon

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ametaka kufanyike uchunguzi wa kina na ulio huru, kuhusu kifo cha mfungwa mwenye miaka 44 - mwanamume raia wa Lebanon Hassan Toufic Dika, kilichotokea tarehe 11 mwezi huu.

Maisha ya maelfu ya raia wa DRC hatarini baada ya kutimuliwa Angola:UN

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa serikali ya Angola kusitisha mara moja zoezi la kuwarejesha kwa nguvu maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokarasia ya Congo DRC, hadi pale itakapohakikishwa kwamba kujeresheshwa huko kunazingatia utawala wa sheria na haki za binadamu za wahamiaji.

Bachelet ahutubia kwa mara ya kwanza Baraza la Haki za binadamu

Kamishna Mkuu mpya wa haki za binadamu wa Umoja wa  Mataifa Michelle Bachelet amehutubia kwa mara ya kwanza kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo huko Geneva, Uswisi na kugusia mambo kadhaa ikiwemo ukiukwaji haki za binadamu dhidi ya warohingywa na huko Syria.

Usiginaji wa haki wafurutu ada duniani:Zeid

Nchi za Afrika ambazo nyingi zimeghubikwa na migogoro , zimefurutu ada kwa usiginaji wa haki za binadamu na hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa kukomesha hali hiyo.

Sauti -
2'54"

Maandamano hayapaswi kuwa uhalifu; Zeid aieleza Iran

Maandamano si uhalifu; Zeid aieleza Iran

Chondechonde Iran shughulikieni kwa uangalifu wimbi la maandamano yanayoendelea nchin humo, amesema Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein katika taarifa yake aliyotoa hii leo.

Sauti -