Ongezeko la machafuko na mashambulizi ya hivi karibuni katika baadhi ya sehemu za Kaskazini Magharibi mwa Nigeria yamewalazimisha watu takribani 20,000 kufangasha virago na kukimbilia Niger kusaka usalama.
Ugumu wa maisha unaowakabili wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, ni moja ya vichocheo vya wazazi kulazimika kuwaoza watoto wao.
Tatizo la ukosefu wa nishati endelevu kwa ajili ya kupikia, limekuwa kikwazo kikubwa kwa jamii ya wakimbizi nchini Tanzania, ambako wanawake na wasichana wamekuwa wakikabiliwa na ubakaji pindi wanapoenda kuokota kuni.