“Ulimwengu unachemka, viongozi ongozeni”: Guterres
Kufuatia ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa WMO kwa kushirikiana na lile la Kamisheni ya Muungano wa Ulaya ambayo imethibitisha kuwa mwezi huu wa Julai utavunja rekodi ya dunia ya kuwa na joto kali ulimwenguni kote, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema takwimu hizi mpya ni uthibitisho kuwa ubinadamu umeketi katika kiti cha moto na kwamba lazima hatua zichukuliwe haraka.