UN yamenzi Rais John Magufuli kwa kupeperusha bendera nusu mlingoti
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, bendera ya Umoja wa Mataifa inapepea kwa nusu mlingoti kuashiria maombolezo ya kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia tarehe 17 mwezi huu wa Machi.
Rais Magufuli aliaga dunia jijini Dar es salaam naamezikwa leo nyumbani kwake huko Chato mkoani Geita nchini Tanzania.