Jean-Pierre Lacroix

Wanawake wana mchango katika amani ya Sudan Kusini

Wanawake nchini Sudan Kusini wameelezwa kuwa na mchango mkubwa katika mchakato wa amani ya taifa hilo lililoghubikwa na vita, hivyo kushirikishwa katika mchakato mzima ni muhimu sana.

Sauti -
3'27"

Bila kushirikisha wanawake amani itakuwa ndoto Sudan Kusini: Lacroix

Amani ya kudumu  na endelevu haitopatikana nchini Sudan Kusini endapo jamii hususan wanawake hawatoshirikishwa katika mchakato wa kuileta. Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa operesheni za ulinzi wa Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix baada ya kukutana na wanawake wakimbizi wa ndani kwenye eneo la Bentiu nchini humo.