Skip to main content

Chuja:

Jamii ya asili

UN News

'Hatuhamihami" bali tunahama na tutarejea- Dkt. Laltaika

Mvutano mkubwa huibuka baina ya wakulima na jamii ya watu wa asili hususan ile ya wafugaji. Mvutano huo ni katika masuala ya matumizi ya ardhi ambapo mara nyingi wafugaji hulaumiwa kutumia ardhi kiholela kutokana na kuhama kwao wanaposaka malisho ya mifugo yao. Umoja wa Mataifa unasisitiza masuala ya matumizi bora ya ardhi kama njia ya kulinda tabianchi Je ni kweli wafugaji  huhamahama? Na je kupitia wafugaji hasa wa jamii ya asili ,dunia inaweza kubadili mweleko wa sasa wa uharibifu wa mazingira na tabianchi. Assumpta Massoi amezungumza na Dkt.

Sauti
4'8"
UN News

Mila zetu za umiliki wa ardhi ndio muarobaini wa mivutano- Jamii ya asili

Jukwaa la kudumu la watu wa asili la Umoja wa Mataifa linakunja jamvi leo Ijumaa huku washiriki wakiweka msisitizo suala la kujumuisha sheria za umiliki wa ardhi za kimila ili kuepuka mizozo ya umiliki wa ardhi za watu wa jamii hiyo.

 

Akihojiwa na Idhaa ya UN kando ya jukwaa hilo, Dk Elifuraha Laltaika, ambaye ni mtaalamu huru wa jukwaa hilo amesema msisitizo huo unazingatia kwamba..

 

(Sauti ya Dkt. Elifuraha Laltaika)

 

Sauti
1'37"