Chuja:

Isaya Yunge

UNNewsKiswahili/Assumpta Massoi

Ubunifu wa spika janja Kaya sasa kuanza kuingia sokoni mwakani

Kila uchao Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushiriki wa vijana katika kuleta mabadiliko katika dunia ya sasa na kuhakikisha mustakabali wa kizazi kijacho unakuwa bora. Umoja wa Mataifa ukitoa wito huo vijana nao wanaitikia kuhakikisha kuwa wanatumia stadi zao kubadilisha maisha ya jamii zao kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Miongoni mwa vijana hao ni Isaya Yunge kutoka Tanzania ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni inayotengeneza spika janja, Smart Kaya.

Sauti
4'26"

13 Septemba 2019

Katika jarida la kina leo hii Flora Nducha anakuletea

-Kenya imezindua rasmi chanjo ya kwanza ya malaria iliyo kwenye majaribio, ugonjwa ambao hukatili maisha ya maelfu ya watu kila mwaka.

-Shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limeonya kwamba hatua za haraka zisipochukuliwa watoto milioni 12 hawatowahi kuonja shule ifikapo 2030

Sauti
10'47"
Isaya Yunge

Vijana changamoto zisiwakatishe tamaa bali ziwape chachu ya kusonga mbele- Isaya

Umoja wa Mataifa hivi sasa unataka vijana ndio wawe mstari wa mbele katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Ndio maana kila uchao kupitia mashirika yake mbalimbali chombo hicho chenye wanachama 193 kinapaza sauti kwa vijana kushiriki na kushirikishwa katika kila utekelezaji wa malengo hayo kuanzia kutokomeza umaskini, kusongesha amani, afya na hata  ubia wa  maendeleo.

Sauti
4'38"