huduma za kujisafi

© UNICEF/Vinay Panjwani

Shule zikiwa zinaanza kufunguliwa, bado hakuna huduma za kujisafi kujikinga na COVID-19- Ripoti

Mjini Mangina jimboni Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mtaalamu wa mradi wa huduma za maji, kujisafi na kunawa mikono, WASH kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF akionesha watoto namna ya kunawa vizuri mikono yao kwa sabuni. 

Huduma hizi ndizo ambazo taarifa ya pamoja iliyotolewa leo huko Geneva, Uswisi na New York, Marekani na mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto, UNICEF na la afya, WHO, yanasema zinakosekana wakati huu shule zinataka kufunguliwa katikati ya janga la COVID-19. 

Sauti
2'53"

13 Agosti 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi 
-  Ripoti ya WHO na UNICEF yasema Shule zikiwa zinaanza kufunguliwa, bado hakuna huduma za kujisafi kujikinga na COVID-19
 - Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO imesema athari mbaya za janga la corona au COVID-19 kwa vijana zimeongeza pengo la usawa na kuhatarisha uwezo wa uzalishaji wa kizazi hicho chote katika jamii. 
-   WFP kupeleka unga wa ngano na nafaka nchini Lebanon  

- Na kwenye makala leo tutaelekea mkoani Morogoro nchini Tanzania kusikia mafan

Sauti
12'40"
UNICEF/Souleiman

Maji safi na salama bado ni ndoto kwa wakazi wengi wa dunia- Ripoti

Ripoti mpya kuhusu pengo la usawa katika fursa ya kupata maji safi ya kunywa na masuala ya usafi  na kujisafi inaonyesha kwamba zaidi ya nusu ya watu wote duniani hawana fursa ya kupata huduma salama za usafi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa leo kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO, na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mabilioni ya watu duniani wanaendelea kutaabika kutokana na kukosa huduma bora za maji na masuala ya usafi.

Sauti
4'22"
Katika makazi ya muda Ain Issa kilometa 50 kaskazini mwa Raqqa nchini Syria, Horriya mwenye umri wa miaka 12 abeba mtungi wa maji.(2017)
UNICEF/Souleiman

Watoto wanoishi katika mizozo wana hatari ya kufa na magonjwa yatokanayo na maji mara tatu zaidi-UNICEF

Watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 wanaoishi katika nchi zilizoathiriwa na mizozo kwa wastani wako hatarini mara tatu zaidi kufa kutokana na magonjwa ya kuharisha yanayosababishwa na ukosefu wa maji salama, huduma ya kujisafi na usafi kuliko matokeo ya ukatili kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na maswala ya watoto, UNICEF.