Hudaydah

Makubaliano ya Stockholm yameleta matokeo chanya kwa kiasi fulani Yemen- Griffiths

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen, Martin Griffiths ameliambia Baraza la Usalama la Umoja huo leo kuwa pande kinzani kwenye mzozo wa Yemen kwa kiasi kikubwa zimezingatia usitishwaji wa mapigano Hudaydah kwa mujibu wa makubalianao yaliyofikiwa mjini Stockholm, Sweden mwaka jana.

Mashauriano huko Sweden kuhusu Yemen yamezaa matunda- Griffiths

Majadiliano ya kisiasa yaliyoratibiwa na  Umoja wa Mataifa  yakihusisha pande mbili katika mzozo wa Yemen yamewezesha mabadiliko katika baadhi ya masuala, amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen, Martin Griffiths akizungumza na waandishi wa habari nchini Sweden.

UN yathibitishwa kusafirishwa kwa wayemen waliojeruhiwa kutoka Sana’a kwenda Oman

Ofisi ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen imethibitisha kusafirishwa kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Sana’a kwenda Muscat, Oman kwa wayemen 50 waliojeruhiwa.

Watoto zaidi ya 60,000 hawasomi, vita vikifunga robo tatu ya shule Hudaydah:

Watoto zaidi ya 60,000 wavulana kwa wasichana hawasomi kwa ajili ya mapigano ndani na katika viunga vya mji wa Hudaydah nchini Yemen.

9 Novemba 2018

Jaridani hii leo Siraj Kalyango anaanzia huko Yemen ambako mashirika ya Umoja wa Mataifa bado yanapaza sauti ya kwamba machafuko  yanayoendelea huko Hudaydah yanakwamisha harakati za usambazaji wa misaada.

Sauti -
12'

Jamani mapigano Hudaydah yakome ili tusaidie wananchi- UN

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na la mpango wa chakula duniani, WFP leo yameelezea hofu yake dhidi y

Sauti -
1'45"

Machafuko yanayoendelea Hudaydah ni changamoto kwa raia na watoa misaada:UNHCR/WFP

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na la mpango wa chakula duniani, WFP leo yameelezea hofu yake dhidi ya kuendelea kwa machafuko kwenye mji wa Hudaydah nchini Yemen na kusema yanaweka njia panda mustakabali wa raia, wakimbizi na operesheni za wahudumu wa misaada ya kibinadamu.

 

Chanjo dhidi ya Kipindupindu yaendelea Yemen

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanashirikiana na serikali ya Yemen katika kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu, OCV, ili kuepusha mlipuko wa tatu wa ugonjwa huo nchini humo.

Yemen! Yemen! Yemen! Pande kinzani malizeni uhasama kwa faida ya raia- WFP

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP David Beasley amezitaka pande zote zinazosigana nchini Yemen kumaliza mgogoro na kuunga mkono amani.

Shambulizi kwenye ghala la chakula latishia uhai wa watu Yemen- WFP

Mapigano katika mji wa bandari wa Hudaydah nchini Yemen ambayo yameharibu ghala la chakula la shirika la mpango wa chakula duniani, WFP yanatishia kudhoofisha jitihada za kulisha mamilioni ya watu katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita, amesema Herve Verhoosel msemaji wa WFP mjini Geneva Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa habari.