HUDAIDAH

Umoja wa Mataifa una wasiwasi na hali inavyoendelea Yemen

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo mjini New York, Marekani kujadili hali ya Yemen ambapo viongozi wakuu wa Umoja wa Mataifa wamelieleza baraza hilo kuhusu wasiwasi wao juu ya machafuko yanayozidi kuongezeka katika maeneo mengine ya Yemen na nje ya mji wa bandari wa Hudaidah ambako mkataba wa kusitisha mapigano unaendelea kutekelezwa.

Watoto wanaendelea kubeba gharama ya vita Yemen licha ya usitishaji uhasama:UNICEF

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, Henrietta Fore amesema vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen vinaendelea kuwabebesha watoto gharama kubwa ya maisha yao.

Utapiamlo bado ni zahma kwa watoto Yemen:UNICEF

Utapiamlo bado ni zahma kubwa nchini Yemen kwa watoto, kina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, ambalo sasa linafanya juhudi kubwa kuhakikisha maelfu ya watoto wanapata lishe inayohitajika kuokoa maisha yao.

Sauti -
1'54"

Bila rasilimali za kutosha WFP haiwezi kufikia watoto ambao maisha yao yako hatarini Yemen

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema licha ya mpango wake wa dharura wa kusambaza chakula nchini Yemen kuwa mkubwa zaidi kuliko yote duniani ukilenga kila mwezi kuwalisha watu milioni 12 wenye njaa kali na walioko hatarini zaidi, bado takribani watu milioni 16 nchini humo wanahaha kupata mlo kila siku kutokana na uhaba wa chakula. 

Shehena ya chakula cha msaada Yemen iko hatarini kuoza- UN

Umoja wa Mataifa umesema suala la la kuyafikia maghala ya shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, yaliyohifadhi shehena ya nafaka huko Hudaidah nchini Yemen linazidi kupata umuhimu zaidi kila uchao.

Pande kinzani Yemen heshimuni makubaliano kuhusu Hudaidah- Baraza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limeridhia kwa kauli moja makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Yemen na wapiganaji wa kihouthi, wakati wa mashauriano yao nchini Sweden wiki iliyopita.

Taswira ya Yemen 2018 ilikuwa ya kutisha lakini kuna nuru 2019- Griffiths

Mwaka 2018 umekuwa mwaka wa 'kutisha' kwa wananchi wa Yemen lakini hata hivyo  unamalizika kwa matumaini kufuatia mazungumzo ya mwezi huu huko Sweden.

Komesheni mauaji ya raia Yemen- Bachelet

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  Michelle Bachelet ameeleza kuchukizwa kwake na ukatili unaoendelea katika mji wa bandari wa Hudaidah, vitendo ambavyo amesema tayari vimesababisha madhila kwa wananchi wengi wa Yemen.

Wayemen wasimulia wanachopitia hadi kupata huduma za afya Sana’a

Nchini Yemen, Umoja wa Mataifa ukiendelea kunusuru wananchi dhidi ya mapigano yanayoendelea kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu hivi sasa, manusura wa mzozo huo wameelezea madhila wanayopata ikiwemo kusaka huduma za afya.

UN yaendelea kuhaha kunusuru wakazi wa Hudaidah nchini Yemen

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema mapigano yanayoendelea hivi sasa kwenye mji wa Hudaidah nchini Yemen yanazidi kuweka hatarini makumi ya maelfu ya watu na kuzuia shirika hilo kuwafikishia misaada ya dharura wanayohitaji