Houthi

Wawaklishi wa serikali ya Yemen na wahouthi wakutana Sweden

Siku ya kwanza ya mashauriano kati ya pande kinzani nchini Yemen ikikamilika huko Rimbo, nchini Sweden, Umoja wa Mataifa umetaja mambo matatu ambayo unatamani yatokane na mkutano huo wa kwanza kabisa kati ya pande hizo baada ya miaka miwili.  Maelezo zaidi na Flora Nducha

Sauti -
2'16"

Serikali ya Yemen na wahouthi wote wanataka mapigano Yemen yakome- Griffiths

Siku ya kwanza ya mashauriano kati ya pande kinzani nchini Yemen ikikamilika huko Rimbo, nchini Sweden, Umoja wa Mataifa umetaja mambo matatu ambayo unatamani yatokane na mkutano huo wa kwanza kabisa kati ya pande hizo baada ya miaka miwili. 

Pande kinzani Yemen zikikutana Sweden, sauti zapazwa ili ziweke mbele maslahi ya watoto

Wawakilishi wa serikali ya Yemen na wale wa kundi la Houthi wakikutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili kwa mazungumzo nchini Sweden hii leo, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen Martin Griffiths amesema fursa hiyo inaleta matumaini ya kuanza tena kwa mchakato wa amani nchini humo.

Komesheni mauaji ya raia Yemen- Bachelet

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  Michelle Bachelet ameeleza kuchukizwa kwake na ukatili unaoendelea katika mji wa bandari wa Hudaidah, vitendo ambavyo amesema tayari vimesababisha madhila kwa wananchi wengi wa Yemen.

La msingi ni kuanza kwa mjadala kuhusu suluhu ya Yemen: Griffins

Mjadala kuhusu kupata suluhu ya mzozo wa Yemen yameanza na ni hatua inayotia matumaini amesema mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo unaondelea nchini humo.

Uhalifu nchini Yemen umetekelezwa na pande zote husika

Pande zote katika mzozo unaoendelea nchini Yemen zimetekeleza na zinaendelea kutekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki na uhalifu chini ya sheria za kimataifa na kusababisha zahma kubwa kwa mamilioni ya raia, limesema leo ripoti ya jopo la wachunguzi lililoteuliwa na Umoja wa Mataifa. 

Sauti -
2'22"

Pande zote katika mzozo Yemen zimetekeleza uhalifu

Pande zote katika mzozo unaoendelea nchini Yemen zimetekeleza na zinaendelea kutekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki na uhalifu chini ya sheria za kimataifa na kusababisha zahma kubwa kwa mamilioni ya raia, limesema leo ripoti ya jopo la wachunguzi lililoteuliwa na Umoja wa Mataifa.

Mazungumzo ya Yemen; serikali na upinzani watumiwa mwaliko

Dalili za kupata suluhu ya mzozo wa Yemen zinaanza kuonekana kufuatia taarifa zinazothibitishwa kuwa Umoja wa Mataifa umewasilisha mwaliko wa  mazungumzo kati ya serikali ya Yemen na wanamgambo wa kihouthi tarehe 6 mwezi  ujao huko Geneva, Uswisi.

Shamubilzi lingine moja tu Hodeidah litakuwa janga lisilozuilika: OCHA

Bandari muhimu nchini Yemen ya Hodeidah ambayo imekuwa ikiandamwa na mashambulizi kutoka kwa vikosi vinavyounga mkono serikali kwa wiki kadha, sasa iko taabani na huenda shambulio linguine moja tu la anga likuka kuwa janga lisilozuilika, kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini humo, OCHA.

Mashambulizi dhidi ya Hodeidah ni sawa na kuua raia- OCHA

Shambulio dhidi ya bandari ya Hodeidah nchini Yemen linaweza kuwa na madhara kwa mamia ya maelfu ya raia wasio na hatia nchini humo ikiwemo kupoteza maisha.