Miaka 80 tangu bomu kuangushwa Hiroshima, Guterres asifu mnepo wa hibakusha
Katika kumbukumbu ya miaka 80 tangu kutokea kwa shambulio la bomu la nyuklia kwenye mji wa Hiroshima, nchini Japani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa akisisitiza umuhimu wa amani, kutokomeza silaha za nyuklia, na kuenzi maisha ya waliopotea na walionusurika.