Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Hepatitis

Upimaji wa homa ya ini Togo
UN

Tunaishi mara moja na tuna ini moja, tutokomeze Homa ya Ini – Dkt. Tedros wa WHO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia ujumbe wake kwa Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini inayoadhimishwa kila Julai 28, amesema kwa kuwa wanadamu tunaishi mara moja na tuna ini moja, WHO imejitolea kushirikiana na nchi zote na wadau wote ili kutimiza maono ya pamoja ya kutokomeza virusi vya homa ya ini ifikapo 2030.  

Sauti
1'59"
Picha: UNICEF/Shehab Uddin

Homa kali ya Ini isiyojulikana yatesa watoto - WHO

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limezindua utafiti duniani kote wenye lengo la kubaini idadi halisi na kiwango cha aina ya ugonjwa wa homa ya ini kali, Hepatitis miongoni mwa watoto, ambao ni tofauti na aina zote za homa ya ini zinazotambulika, wakati huu ambao ugonjwa huo umeripotiwa katika kanda 5 za WHO isipokuwa barani Afrika. Leah Mushi na maelezo zaidi. 

Sauti
2'20"

13 JULAI 2022

Hii leo katika jarida tunamulika utafiti ambao WHO inafanya ili kubaini aina mpya ya ugonjwa wa homa ya ini kali au Hepatitis B ambayo inakumba watoto, ugonjwa umepatikana kanda zote za WHO isipokuwa Afrika. Kisha tunakwenda Haiti kuangazia changamoto za kiuchumi, kijamii na kiusalama lakini Umoja wa Mataifa haukati tamaa unaendelea kupeleka misaada ya kibinadamu .Makala inammulika Priscilla Lecomte, raia huyu wa Ufaransa ambaye anazungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha na sasa naona nafasi kubwa ya lugha hiyo katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Sauti
10'13"
Chanjo dhid ya homa ya Ini aina ya B Argentina
Photo: WHO/PAHO

WHO kuchunguza kuenea kwa homa kali ya ini isiyojulikana

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limezindua utafiti duniani kote wenye lengo la kubaini idadi halisi na kiwango cha aina ya ugonjwa wa homa ya ini kali, Hepatitis miongoni mwa watoto, ambao ni tofauti na aina zote za homa ya ini zinazotambulika, wakati huu ambao ugonjwa huo umeripotiwa katika kanda 5 za WHO isipokuwa barani Afrika.

Sauti
2'20"