Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, ikiwa inaghubikwa na janga la kibinadamu la muda mrefu duniani, Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Henrietta H.Fore na Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, Mark Lowcock leo kwa pamoja wametoa wito wa kuisaidia DRC kufikia mahitaji ya watoto, familia na jamii zilizoko hatarini wakiwemo watu wenye ulemavu, taarifa iliyotolewa mjini Kishasa, New York Marekani na Geneva Uswisi imeeleza.