Hapa na pale

Afghanistan yaingia mkatana na UM kutoingiza watoto jeshini

Umoja wa Mataifa na serikali ya Afghanistan wametia sahihi makubaliano ambapo Afghanistan ilikubali kusaiadia watoto walioathirika na mizozo na pia kuzuia kuingizwa watoto kwenye jeshi.

Ban azungumza na viongozi wa Rwanda na Ufaransa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Ufaransa na Rwanda ambako wamejadilia masuala mbalimbali ikiwemo shabaya ya Umoja huu wa Mataifa kuendelea kushirikiana na mataifa hayo.

IOM kutafiti athari za fedha zinazotumwa nyumbani Pakistan

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezindua utafiti wa kutaka kubaini athari za fedha zinazotumwa nyumbani na wafanyikazi wahamiaji raia wa Pakistan wanaofanya kazi nchini Saudi Arabia kwa familia zao nyumbani.

UNHCR yakaribisha sheria mpya ya wakimbizi Mexico

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua iliyochukuliwa na serikali ya Mexico kupitisha sheria mpya inayowalinda wakimbizi pamoja na wale wanaoomba hifadhi.

Nchi zilizokumbwa na migogoro zisaidiwe:UM

Nchi ambazo zilikumbwa na migogoro na machafuko ya mara kwa mara lakini sasa zimeanza kuchipua upya zinapaswa kuungwa mkono na kupewa usaidizi wa hali ya juu na jumuiya zote za kimataifa.

Nategemea serikali mpya Lebanon kutoa ushirikiano:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anatumai kuwa serikali mpya ya Lebanon itatoa ushirikiano wa dhati kwa mahakama maaalumu inayoendesha uchunguzi juu ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Rafiq Hariri aliyeuwawa mwaka 2005.

UM washangazwa na dhuluma dhidi ya watoto Ivory Coast

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya watoto na mizozo ameelezea kushangazwa kwake kufuatia kuendelea kwa ghasia nchini Ivory Coast yakiwemo madai ya mauaji , kuwalemaza na utekaji nyara wa watoto tangu kuanza kwa mzozo nchini humo.

IOM na Lao kupambana na ugonjwa wa TB kwa wahamiaji

Shirika la kimataifa la uhamaiji IOM kwa ushirikiano na wizara ya afya nchini Lao wamezindua mradi wa mwaka mmoja wa kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu miongoni mwa jamii ndogo na wahamiaji nchini humo.

Miundombinu ni kikwazo cha kuwafikia wakimbizi Liberia:UNICEF

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa asilimia 85 ya wakimbizi wanaoingia nchini Liberia kutoka Ivory Coast ni watoto na wanawake.

UM una jukumu la kukemea uvunjaji wa haki za binadamu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Umoja huo ndiyo wenye dhamana ya kukemea na kuzungumzia hadharani vitendo vyovyote vya uvunjivu wa haki za binadamu na kuwapa sauti wale wanaoonewa.