Hapa na pale

Haiti inapaswa kumteua Waziri Mkuu haraka iwezekanavyo:UM

Haiti inapaswa kumteua Waziri Mkuu haraka iwezekanavyo ili kuepusha hali yoyote ya mkwamo inayoweza kujitokeza.

Sauti -

MONUSCO yapokea msaada wa Helkopta toka Ukraine

MONUSCO yapokea msaada wa Helkopta toka Ukraine

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vinavyoendesha operesheni yake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, vimepokea helkopta moja toka kwa serikali ya Ukraine ambayo itasaidia kuimarisha shughuli zake kwenye eneo hilo.

Sauti -

Mahiga ataka kuwe na usawa wa kijinsia na kuwajumuisha wanawake kwenye masuala muhimu

Mahiga ataka kuwe na usawa wa kijinsia na kuwajumuisha wanawake kwenye masuala muhimu

Siku ya kiamataifa ya wanawake ikiadhimishwa hii leo ofisi inayohusika na masuala ya kisiasa ya Umoja wa mataifa kuhusu Somalia UNPOS imeonyesha uzalendo wake kwa wanawake kote duniani hasa walio kwenye maeneo yanayokabiliwa na mizozo na kuunga mkono jitihada za wanawake za kuleta amani nchini
Sauti -

Somalia yaomba kuingia Afrika Mashariki:

Somalia yaomba kuingia Afrika Mashariki:

Somalia ambayo imekua ikijaribu kujikwamua toka vita vya miaka 20 imetuma maombi yakutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 Kenya ambayo ndio mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo imethibitisha kupokea maombi ya Somalia.

Sauti -

Ban ataka vizingiti vinavyomkwaza mwanamke kiuchumi viondolewe

Ban ataka vizingiti vinavyomkwaza mwanamke kiuchumi viondolewe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuondolewa vizuizi na vikwazo vinavyowaandama wanawake duniani kutojitokeza kwenye masuala ya ukuzaji uchumi.

Sauti -