Hapa na pale

Nchi zaidi zimetia sahihi mkataba kulinda bayo-anuai

Colombia, Denmark, Netherlands na Sweden zimekuwa nchi za kwanza kutia sahihi mkataba mpya kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ulio na sheria za kimataifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa iwapo kutaokea uharibifu kwenye balojia anuai na viumbe unaosababishwa na viumbe vilivyofanyiwa mabadiliko ya kimaumbile.

Ushahidi unaopatikana kwa njia ya mateso upuuzwe:UM

Mtaamu huru wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya mateso ametaka ushahidi unaopatikana baada ya kufanyika vitendo vya kuwatesa watuhumiwa usipewe uzito wowote tena.

Matumizi ya nyuklia yaongezeka duniani:IAEA

Nchi nyingi duniani hivi sasa zinageukia nyuklia kama chanzo cha nishati amesema mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA.

Uchunguzi ufanyike kuhusu mashambulizi Afghanistan:Coomaraswamy

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na watoto pamoja na maeneo yaliyokumbwa na mizozo ya vita,ametaka kuwepo kwa uchunguzi kufuatia vikosi vya jumuiya ya kujihami NATO kufanya shambulizi huko Kaskazini mwa Afghanistan na kuuwa watoto tisa.

UM waiomba radhi Belarus kwa kuituhumu kukiuka vikwazo vya silaha

Umoja wa mataifa umeomba radhi serikali ya Belarus ambayo hapo awali ilituhumiwa

kuwa ilikiuka vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa kwa utawala Laurent Gbagbo wa

Ivory Coast, aliyepigwa marafuku kusambaziwa silha za aina yoyote.

UM wazindua ofisi kuzisaidia nchi za Afrika ya Kati

Umoja wa mataifa leo umefungua ofisi maalumu kwa ajili ya kutoa msukumo wa

kisiasa kwa kuimarisha hali ya amani na kuzua uwezekano wa kutokea machafuko

katika nchi za afrika ya kati.

Makubaliano ya Cancun yatekelezwe kwa vitendo:Figueres

Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na hali ya hewa, ameyatolea mwito mataifa duniani kuharakisha utekelezaji kwa vitendo makubalino yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Cancun na wakati huo huo ametaka mataifa hayo kuanisha njia mbadala itakayoanisha mustabala wa itifaki ya Kyoto inayohimiza mapinduzi ya kijani.