haki za binadamu

Bi. Bachelet ni gwiji wa masuala ya haki za binadamu- Guterres

Mabibi na mabwana, nina furaha kubwa kutangaza kuwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeridhia uteuzi wangu wa Michelle Bachelet kuwa Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa  Umoja wa Mataifa!

Sauti -
2'58"

Nicaragua sitisha hatua za kuwaandama wapinzani- Wataaalam wa UN

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameihimiza serikali ya Nicaragua ikomeshe ukandamizaji kufuatia siku 100 za maandamano ambapo watu  takriban 317 wameuawa ilhali wengine 1,830 wamejeruhiwa.

Watakaohusishwa na unyanyasaji wa kingono hawana kazi UNHCR

Pamoja na jitihada za kupiga vita unyanyasaji wa kingono na ukatili, dhidi ya waathirika wa kivita katika maeneo ya migogoro  duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,

Sauti -
1'28"

Haki za watoto zinaendelea kusiginwa Palestina na kututia hofu kubwa-UN

Umoja wa Mataifa umesema unatiwa hofu kubwa na kuendelea kukiukwa kwa haki za watoto kwenye maeneo yanayokaliwa ya Wapalestina, na kutaka hatua muhimu na za haraka kuchukuliwa ili kuruhusu watoto kuishi kwa uhuru bila hofu na kufurahia haki zao.

Kenya sitisheni kuwafurusha wakazi wa Kibera si haki:UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani hatua ya serikali ya Kenya ya kuwafurusha wakazi wa mitaa ya mabanda ya Kibera mjini Nairobi na kuitaka serikali kusitisha mara moja zoezi hilo hadi pale hatua za kisheria zitakapokamilika.

Haki ni haki lazima Kenya izingatie hilo:Wataalam

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na haki za binadamu zihusuzo masuala ya kibiashara wameitaka serikali ya Kenya kutimiza wajibu kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 nchini humo na kuhakikisha masuala ya biashara yanatimiza haki za binadamu, kwani haki ni haki lazima itimizwe.

Sauti -
2'11"

Kenya hakikisha sekta ya biashara inazingatia haki za binadamu- Wataalam 

Kikundi kazi cha wataalam wa Umoja wa Mataifa juu ya biashara na haki za binadamu kimehimiza mamlaka nchini Kenya kutekeleza kwa vitendo mapendekezo yaliyotajwa katika Katiba ya nchi hiyo ya 2010 ya kuhakikisha biashara zinaheshimu haki za binadamu.

Bado haki za binadamu zinakiukwa Eritrea:Keetharuth

Mtaalamu maalum wa umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu  nchini  Eritrea,  ameelezea wasiwasi wake kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo pamoja na mvutano wa mpaka unaondelea kati ya Eritrea na jirani yake Ethiopia.

Venezuela imeshindwa kuwawajibisha wakiukaji wa haki za binadamu:UN Ripoti

Serikali ya Venezuela imeshindwa kuwawajibisha wakiukaji wa kubwa wa haki za vinadamu ikiwemo mauaji, matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, watu kuswekwa rumande kinyume cha sheria, ukatili na mateso.

Kiswahili ni lugha ya taifa na kila mtoto ikiwemo walio na ulemavu wafundishwe-Seneta Inimah

Kuwa mlemavu sio kulemaa na unastahili kupata haki zote kama wengine , iwe elimu, afya na hata kutoachwa nyuma katika malengo ya maendeleo endelevu au SDG's, amesema seneta wa Kenya ambaye yeye mwenyewe ni mtu mwenye ulemavu.