haki za binadamu

Fursa ya utoaji mimba salama yahitajika kuokoa wanawake 47,000 kila mwaka:UN

Nchi zote duniani zinapaswa kuchukua hatua sasa kutoharamisha utoaji miamba na kuhakikisha wanawake na wasichana wana haki ya kufanya maamuzi kuhusu hali ya ujauzito , wamesema wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa .

Hongera Sudan Kusini kwa kuchukua hatua zaidi kuwalinda watoto:Gamba

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto na migogoro ya Silaha, Bi. Virginia Gamba, ameipongeza serikali ya Sudan Kusini kwa kuongeza kipengele cha hiyari kwenye mkataba kuhusu haki za mtoto katika ushirikishaji kwenye migogoto ya kivita (OPAC).

Haki za binadamu ni chombo cha kumuendeleza mwanadamu: Guterres

Kauli ya kuwa masuala ya haki za binadamu  duniani yamepitwa na wakati na badala yake   utaifa ndio kitu muhimu kinachopashwa kupewa msisitizo  imepingwa na baadhi ya viongozi ambao wanakutana mjini New York Marekani kuzindua  jukwaa lililopatiwa jina “habari njema za haki za binadamu.”

Bado haki za binadamu zimesalia ndoto kwa wakazi wengi duniani- UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema miaka ya 70 ya tamko la haki za binadamu duniani, haijawa tiketi kwa kila mtu kufarahia haki za msingi zilizoainishwa katika nyaraka hiyo.

Wahanga na watetezi wa haki za binadamu wanaadhibiwa vikali:UN

Watu kote duniani wanakabiliwa na adhabu na vitisho vikubwa kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika masuala ya kupigania haki za binadamu, jambo ambalo ni “aibu kubwa” imeonya leo ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Vijana wasanii wana silaha ya kuchagiza haki za binadamu katika jamii zao

Sanaa ni moja ya mbinu inayoweza kutumika katika jamii kufikisha ujumbe na kuchagiza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu ikiwemo lengo la haki za binadamu, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. John Kibego na tarifa kamili

Sasa nimeelewa tamko la haki za binadamu ni sawa na sheria mama- Kijana kutoka Tanzania

Umoja wa Mataifa unaendelea kutumia kila mbinu huko mashinani kuhakikisha misingi na malengo yake vinafahamika vyema miongoni mwa siyo tu mamlaka bali pia wananchi.

Sauti -
4'29"

UNIC Tanzania yanoa wachora vibonzo ili waeneze haki za binadamu

Suala la haki za binadamu ni moja ya misingi ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka 1945. Na ndio maana chombo hicho kilipitisha tamko la haki za binadamu lililo msingi wa katiba, kwa nchi zilizoridhia nyaraka hiyo ikiwemo zile za Afrika Mashariki.

Sauti -
3'49"

Machungu ya raia ndio kichocheo changu cha kupaza sauti- Zeid

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema machungu wanayopitia wahanga wa ukiukwaji wa haki  za binadamu ni shinikizo kubwa kwake yeye kuzungumza bila woga.

Simulizi ya wasichana wanne walionyimwa haki zao ilitutoa sote machozi- Zeid

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema machungu wanayopitia wahanga wa ukiukwaji wa haki  za binadamu ni shinikizo kubwa kwake yeye kuzungumza bila woga. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Sauti -
2'25"