haki za binadamu

Ukiukwaji na mauaji ya kimbari dhidi ya Rohingya vinaendelea Myanmar:Darusman

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Mataifa ya kutafuta ukweli wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Myanmar, Marzuki Darusman amesisitiza kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya kimbari vinaendelea dhidi ya jamii ya watu wa kabila la Rohinya.

Vita dhidi ya ugaidi sio sababu ya kubinya uhuru wa dini au imani:Shaheed 

Haki ya uhuru wa dini au imani ni suala mtambuka ambalo mara nyingi halieleweki vyema na kusababisha haki hiyo kukiukwa kwa kiasi kikubwa kote duniani.

Uwajibikaji ndio msingi wa upatanisho Myanmar:Burgener

Uwajibikaji na majadiliano jumuishi ni mihimili miwli muhimu katika maridhiano ya kitaifa nchini Myanmar, amesema mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Schaner Burgener katika taarifa yake iliyotolewa Jumamosi.

Saudi Arabia achilia huru wanaotetea haki za wanawake- Wataalam

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, wanaihimiza Saudi Arabia iwaachilie huru  mara moja na bila ya masharti yoyote watetezi wote wa haki za binadamu za wanawake wakiwemo watetezi sita wanaoshikiliwa kwa  madai ya kuhusika na utetezi wa haki za binadamu waliofanya kwa amani

Tunatiwa hofu na kushikiliwa kwa raia wa Colombia nchini Venezuela:UN

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa hofu na kitendo cha raia 59 wa Colombia kuendelea kushikiliwa mahabusu nchini Venezuela bila kufunguliwa mashitaka yoyote kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

 

Serikali sikilizeni watoto wa kike na wapatieni haki zao- Wataalam

Kuelekea siku ya mtoto wa kike tarehe 11 mwezi huu wa Oktoba, wataalamu wa haki za binadmu wa Umoja wa Mataifa wametaka serikali kote duniani zisikilize sauti za watoto wa kike na wasichana kama njia mojawapo ya kuwapatia haki zao za msingi.

Mauaji ya wanahabari wanawake yamefurutu ada:UNESCO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO amelaani vikali mauaji ya kikatili ya Victoria Marinova , muandishi wa habari wa televisheni ambaye maiti yake ilikutwa mjini Ruse Bulgaria Oktoba 6 ikiwa na dalili za kuteswa kufanyiwa ukatili wa kingono.

Heri nusu shari kuliko shari kamili ya mabadiliko ya tabia nchi:UN

Mtihani wa mabadiliko ya tabia nchi ni mkubwa lakini ni wajibu wa kila mtu na kila nchi kuchukua hatua sasa kuepuka janga lenye gharama kubwa hapo baadaye, umeonya Umoja wa Mataifa. Kiwango cha joto kinaongezeka  na athari ni pamoja na haki za binadamu za afya, chakula, maji na mazingira.

Sauti -
2'29"

Fursa ya utoaji mimba salama yahitajika kuokoa wanawake 47,000 kila mwaka:UN

Nchi zote duniani zinapaswa kuchukua hatua sasa kutoharamisha utoaji miamba na kuhakikisha wanawake na wasichana wana haki ya kufanya maamuzi kuhusu hali ya ujauzito , wamesema wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa .

Hongera Sudan Kusini kwa kuchukua hatua zaidi kuwalinda watoto:Gamba

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto na migogoro ya Silaha, Bi. Virginia Gamba, ameipongeza serikali ya Sudan Kusini kwa kuongeza kipengele cha hiyari kwenye mkataba kuhusu haki za mtoto katika ushirikishaji kwenye migogoto ya kivita (OPAC).