haki za binadamu

Kenya sitisheni kuwafurusha wakazi wa Kibera si haki:UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani hatua ya serikali ya Kenya ya kuwafurusha wakazi wa mitaa ya mabanda ya Kibera mjini Nairobi na kuitaka serikali kusitisha mara moja zoezi hilo hadi pale hatua za kisheria zitakapokamilika.

Haki ni haki lazima Kenya izingatie hilo:Wataalam

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na haki za binadamu zihusuzo masuala ya kibiashara wameitaka serikali ya Kenya kutimiza wajibu kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 nchini humo na kuhakikisha masuala ya biashara yanatimiza haki za binadamu, kwani haki ni haki lazima itimizwe.

Sauti -
2'11"

Kenya hakikisha sekta ya biashara inazingatia haki za binadamu- Wataalam 

Kikundi kazi cha wataalam wa Umoja wa Mataifa juu ya biashara na haki za binadamu kimehimiza mamlaka nchini Kenya kutekeleza kwa vitendo mapendekezo yaliyotajwa katika Katiba ya nchi hiyo ya 2010 ya kuhakikisha biashara zinaheshimu haki za binadamu.