haki ya binadamu

Ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni vimetawala Uingereza :Achiume

Sera za serikali ya Uingereza zinachochea ubaguzi wa rangi , chuki dhidi ya wageni na kuongeza hali ya kutokuwa na usawa kwa misingi ya rangi kwa mujibu wa  ripoti ya mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi na haki za binadamu.

ILO hakikisheni uwepo wa mazingira salama na yenye afya kazini:UN

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu hii leo wamelitaka Shirika la Kazi Duniani ILO mara moja kutambua na kuanza kutekeleza suala la mazingira salama na yenye afya kazini kama moja ya haki za kimsingi kazini.

Cambodia achia huru mliowakamata wakati wa uchaguzi- OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, imesema ina wasiwasi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Cambodia kufuatia ripoti ya kwamba uchaguzi mkuu  ulifanyika mwishoni mwa mwezi uliopita bila ushiriki wa chama kikuu cha  upinzani cha CNRP kilichofutwa.

Watakaohusishwa na unyanyasaji wa kingono hawana kazi UNHCR

Pamoja na jitihada za kupiga vita unyanyasaji wa kingono na ukatili, dhidi ya waathirika wa kivita katika maeneo ya migogoro  duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR sasa limegeuzia harakati hizo kwa wafanyakazi wake ili  kutokomeza vitendo hivyo viovu.

Haki za waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu ni lazima zizingatiwe:UN

Haki za waathirika wa biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu hususan wanawake na watoto zinapaswa kuzingatia , na nchi ni lazima zinafanye kila njia kuzuia na kupambana na janga hili la kimataifa.

Kila mtu ana haki ya uzazi wa mpango:UNFPA

Uzazi wa mpango ni haki ya binadamu na hivyo kila mtu ana haki ya kuchagua ni watoto wangapi anataka kuwa nao na watapishana umri wa kiasi gani, umesisitiza leo Umoja wa Mataifa ukiadhimisha siku ya idadi ya watu duniani.

Sauti -
3'

Myanmar achia huru waandishi wa habari wa Reuters -UN

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wana wasiwasi baada ya  mahakama nchini Myanmar kuwafungulia rasmi mashtaka waandishi wa habari wawili wa shirika la habari la Reuters.