Habari za wiki

Amani itapatikana Afrika Magharibi kwa kuwapokonya silaha wapiganaji

Baraza la usalma la Umoja wa Mataifa wiki hii limesema upokonaji silaha na kuwarudisha katika maisha ya kawaida wapiganaji wa zamani na kukomesha tatizo kubwa la biashara haramu ya silaha ndogo ndogo ni hatua muhimu kabisa ambazo nchi za Afrika ya Magharibi zinabidi kuchukua ikiwa amani itadumishwa katika eneo hilo.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu aridhishwa na juhudi za kuleta amani nchini Somalia

Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Somalia amesema ameridihika kusikia ripoti kua juhudi za Ethiopia za kupatanisha ugomvi katika serekali ya mpito ya Somalia imeonesha ishara za kufanikiwa.

Umoja wa Mataifa kulaani mashambulio nchini Burundi

Umoja wa Mataifa umelaani vikali mashambulio yanayotokea huko Burundi mnamo wiki hii ambapo mfanya kazi mmoja wa Umoja wa Mataifia alijeruhiwa.

Matokeo ya muda ya uchaguzi yazusha wasiwasi DRC

TMY:Matokeo mengine muhimu kwa wiki hii ni hali baada ya uchaguzi wa kihistoria ya huko jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Wakuu wa UM wanataka Wa-Kongo wasubiri matokeo rasmi

Likiwapongeza wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kushiriki katika uchaguzi wa kihistoria wa nchi yao, kwa sehemu kubwa kabisa kwa amani, siku ya Jumapili, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa mwito wiki hii kuwataka wawe watulivu na kusubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

IGAD yaunga mkono sera za Umoja wa Mataifa Somalia

Mjumbe maalum wa UM huko Somalia, Francois Lonseny Fall, amepongeza tangazo la sera lililotolewa na mawaziri wa nchi za mamlaka ya maendeleo ya pembe na Afrika ya mashariki IGAD, likidai kufuata sera za UM huko Somalia.

Jaribio la Mapinduzi lagunduliwa Burundi

Afisi ya kulinda amani ya UM huko Burundi ONUB imeeleza kushangazwa na ripoti kua kulikuwepo na jaribio la kuipindua serekali ya Bujumbura, siku chache zilizopita na kwamba kuna wanasiasa mashuhuri walotiwa vizuizini.

UNICEF kulaani vitendo vya ubakaji wa watoto Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limelaani vikali sana habari za kutokea vitendo zaidi vya ubakaji huko Zimbabwe na likihimiza sheria mpya kupitishwa kuwalinda watoto wa nchi hiyo na kutoa masomo zaidi juu ya virusi vua HIV na Ukimwi.

Wanajeshi waangalizi wanne wa UM Kuuwawa Lebanon

Naibu KM wa Idara ya UM juu ya Operesheni za Amani Duniani, Jane Holl Lute aliripoti mbele ya Baraza la Usalama wiki hii kwamba wanajeshi waangalizi wanne wa ulinzi wa amani wasiochukua silaha kutoka Austria, Kanada, Finland ~na Uchina, waliuawa Ijumanne kwa mizinga ya majeshi ya Israel ambayo tuliarifiwa ililengwa moja kwa moja, sawia, kwenye kituo cha uangalizi cha UM karibu na mji wa Khiam, Lebanon ya kusini.

UM yaahidi kuongeza misaada ya kiutu Lebanon

Ilivyokuwa matatizo ya kiutu bado yanaendelea kukithiri katika mazingira ya vita katika Lebanon ya kusini UM umeripoti ya kuwa utalazimika kupeleka misafara ziada ya misaada ya kihali katika miji ya Jezzine na Sidon ili kukidhia mahitaji ya kunusuru maisha kwa umma waathiriwa wa maeneo haya. Hatua hii imechukuliwa baada ya msafara wa UM kufanikiwa Ijumanne kupeleka katika mji wa bandari wa Tyre shehena za chakula na mahitaji mengineyo ya kiutu.