Habari za wiki

Baraza la Usalama kupeleka jeshi la kulinda amani nchini Sudan

Baraza la Usalama, limekubali kupeleka jeshi la kulinda amani la Umoja wa mataifa la zaidi ya wanajeshi elfu 17 katika jimbo lenye ghasia la Darfur huko Sudan, ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Bw. Kingsley kuzionya serikali za Chad na Sudan kutanzua tofauti kati yao

Mratibu wa huduma za dharura wa Umoja wa mataifa huko Chad, ambako kuna maelfu na maelfu ya wakimbizi wa Kisudan kutoka jimbo la Darfur, ameonya kwamba kutaweza kutokea maafa makubwa ya kibinadamu, ikiwa serekali za nchi hizo mbili hazitotanzua tofauti kati yao na kutafuta njia za kusitisha ghasia.

Njia za kudumisha amani na maendeleo nchini Somalia

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu huko Somalia Bw Francois Fall alikutana na kundi la wajumbe wa kimataifa linalo jaribu kutafuta njia za kudumisha amani na maendeleo katika taifa hilo la pembe mwa afrika na kujadili njia za kuimarisha msaada wa kimataifa katika juhudi zao

Wagombea urais nchini DRC wakubali kuunda tume

Afisi ya Umoja wa mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUC ilitangaza wiki hii kuwa wagombea wawili walobaki wa kiti cha rais huko kutokana na uchaguzi wa mwezi uliyopita, wamekubaliana kuunda tume ya pamoja kuchunguza ghasia zilizotokea baada ya kutolewa matokeo ya awali,

Maendeleo makubwa kupatikana nchini Sierra Leone

Kufuatana na ripoti mpya ya Katibu Mkuu Koffi Annan, kwa Baraza la Usalama, ni kwamba licha ya maendeleo makubwa yaliyopatikana, Sierra Leone inakabiliwa na matatizo na vitisho muhimu katika usalama wake

Sudan kupata huduma za afya kutoka serikali ya Japan

Akina mama na watoto wa kaskazini mwa Sudan watafarijika hivi sasa kwa kuweza kupata machanjo muhimu ya kuokoa maisha na madawa ya malaria pamoja na huduma za afya kutokana na msaada kutoka serekali ya Japan wa dola milioni 4.5 ulokabidhiwa UNICEF. Shirika la watoto linaeleza kua msaada huo utasaidia kuimarisha afya ya kiasi ya watu milioni 3 na nusu.

Wasi wasi kutokana na kutangwaza maneno ya chuki dhidi ya wazungu huko DRC

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Bwana Willam Lacy Swing ameeleza wasi wasi mkubwa kutokana na kutangazwa maneno ya chuki dhidi ya wazungu kwenye vyombo vya habari.

Baraza la Usalama lapitisha azimio juu ya mapigano kati ya Israel na Lebanon

Juhudi za kidiplomasia zinaendelea katika Baraza la Usalama na katika miji mikuu ya nchi mbali mbali kujaribu kutafuta suluhisho la kusitisha mapigano kati ya Israel na wapiganaji wa Hezbollah huko Lebanon.

Amani itapatikana Afrika Magharibi kwa kuwapokonya silaha wapiganaji

Baraza la usalma la Umoja wa Mataifa wiki hii limesema upokonaji silaha na kuwarudisha katika maisha ya kawaida wapiganaji wa zamani na kukomesha tatizo kubwa la biashara haramu ya silaha ndogo ndogo ni hatua muhimu kabisa ambazo nchi za Afrika ya Magharibi zinabidi kuchukua ikiwa amani itadumishwa katika eneo hilo.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu aridhishwa na juhudi za kuleta amani nchini Somalia

Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Somalia amesema ameridihika kusikia ripoti kua juhudi za Ethiopia za kupatanisha ugomvi katika serekali ya mpito ya Somalia imeonesha ishara za kufanikiwa.