Habari za wiki

Waandishi habari wanaofanya kazi kwenye maeneo ya vita walindwe: UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ambalo pia linapigania uhuru wa habari na wa kujieleza leo limetoa wito wa kuimarisha usalama kwa waandishi na wafanyakazi wengine wa sekta ya habari wanaofanya kazi kwenye maeneo ya vita au machafuko ya kijamii.

Asilimia 25 tuu ya msaada wa kipindupindu Haiti ndio umepatikana: UM

Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema tatizo la kipindupindu Haiti halijamalizika huku msaada ulioombwa kukabiliana na ugonjwa huo umepatikana asilimia 25 tuu.

Bunge la Puntland kujadili ujenzi wa Ghala la WFP

Bunge la Puntland leo limejadili rasmi unjezi wenye utata wa ghala la shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP karibu na uwanja wa ndege wa Boosaaso.

WFP kupunguza tatizo la chakula kwa kununua ngano Afghanistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limesema litaweza kusaidia tatizo la upungufu wa ngano nchini Afghanistan kwa kununua ngano hiyo kwa kiwango kibubwa nchini humo.

Baraza la Haki za Binadamu kukutana kujadili hali ya Ivory Coast

Wakati huohuo baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kesho Alhamisi Desemba 23 itafanya kikao maalumu kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Ivory Coast tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu Novemba 28.

Ivory Coast inatia iko katika hatihati ya vita tena:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonya kwamba kuna hatari kubwa ya kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ivory Coast.

Serikali mpya ya Iraq ni hatua kubwa katika demokrasia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekaribishwa kutangazwa kwa serikali mpya mjini Baghdad na kusema ni hatua kubwa kuelekea mchakato wa demokrasia nchini Iraq.

Vijana waongoza ajenda kwenye mkutano wa baraza la usalama la UM

Vijana kutoka kote duniani wameelezea mtazamo wao kuhusu masuala wanayoayona kuwa muhimu kwenye mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York leo.

Mwaka wa Bayo-Anuai umemalizika kwa mafanikio na kuundwa chombo kipya: UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linasema chombo kipya cha kimataifa chenye lengo la kukabiliana na kupotea kwa bayo-anuai, misitu muhimu kiuchumi duniani, viumbe vingine vya majini kimezaliwa jana, baada ya muafaka wa serikali na mkutano wa 65 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Baridi kali iliyoikumba Ulaya kupungua kidogo: WMO

Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kwamba hali ya baridi kupindulia inayoathiri sehemu za Ulaya Magharibi na Mashariki mwa Marekani itapungua katika siku chache zijazo.