Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura, Ursula Mueller, amesema hali bado ni tete nchini Syria kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa zaidi ya miaka saba sasa.
Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kumeanza jukwaa la vijana kutoka nchi wanachama wa umoja huo, wakiweka bayana kile wanachoona ni muhimu kwa mustakhbali wao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA limezindua harambee ya kuchangisha fedha zaidi ya dola millioni 800 kwa wapalestina walioko katika eneo linalokaliwa la Gaza na ukingo wa magharibi wa mto Jordan. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.
Pata muhtasari wa kile kitakachokuwemo katika wavu wetu mpya utakaozinduliwa rasmi tarehe 01 Februari mwaka huu wa 2018. Halikadhalika fahamu sababu za kuleta wavuti huu mpya. Wenyeji wako ni Flora Nducha na Siraj Kalyango.
Mkutano wa kawaida wa 30 wa viongozi wa Afrika ukiendelea huko Addis Ababa, Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja mambo matano ya kuimarisha ushirikiano kati a pande mbili hizo.