Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon Michael Williams leo ametoa wito wa kuundwa haraka serikali mpya nchini humo akisema ni muhimu sana kwa usalama na maendeleo ya watu wa taiafa hilo.
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na serikali ya Kenya wamendaa kongamano la amani lililo na lengo la kuboresha uhusiano kati ya jamii ya Turkana nchini Kenya na Tuposa nchini Sudan.
Serikali ya Somalia inayoungwa mkono bna Umoja wa Mataifa umeongeza muda wake kupokea udhamini kwa mwaka mmoja zaidi hata baada ya kupokea shutuma kutoka kwa wafadhili na mashambulizi inayokabiliana nayo kutoka kwa wanamgambo.
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema kuwa mapigano makali yameripotiwa katika maeneo ya magharibi mwa Ivory Coast na kusababisha kukwama kwa maelfu ya watu waliokimbia makwao.
Shirika la afya duniani WHO kwa ushirikiano na wizara ya afya nchini Misri wanaendesha shughuli za kuwahamisha waliojeruhiwa kwenye mapigano yanayoendelea nchini libya ili wapate matibabau.
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo ameonya kwamba mapigano yanayoendelea Yemen yanazidisha adha kwa hali ambayo tayari ni mbaya, na amezitaka pande zote kusitisha machafuko.
Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika, umebaini kwamba vijiji kadhaa Kaskazini mwa Darfur Sudan eneo vilivyoshuhudia mapigano makali mapema mwezi huu baina ya majeshi ya serikali na waasi vimetelekezwa.