Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio lililofanyika leo kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul ambako washambuliaji walitumia gari linalofanana na gari la wagonjwa kutekeleza shambulio hilo.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya halaiki dhidi ya wayahudi, Umoja wa Mataifa umesema silaha pekee dhidi ya vitendo kama hivyo ni elimu na uelewa kuhusu maadili ya kibinadamu.
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, amezindua mkakati wa kushughulikia zahma ya kibinadamu mwaka huu wa 2018 nchini Libya.
Mataifa yenye maendeleo duni zaidi duniani yako mbioni kumudu kuwa na mtandao wa mawasiliano ya intaneti ifikapo mwaka 2020 kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo. Ripoti hiyo iliyotolewa na muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU inasema nchi zenye maendeleo duni au LDC’s zinapiga hatua kubwa katika kufikia fursa ya habari na teknolojia ya mawasiliano.