guara guara

Manusura wa Idai Msumbiji wahamishiwa karibu na nyumbani

Maelfu ya manusura wa kimbinga Idai nchini Msumbiji wameanza kuhamishiwa katika maeneo ya mwinuko yaliyo karibu na nyumbani walikokuwa kabla ya kimbunga.

Sauti -
1'36"

Manusura wa IDAI wasogezwa karibu na nyumbani - UNHCR

Familia zilizonusurika na kutawanywa na kimbunga Idai nchini Msumbiji zimeanza kuhamishiwa katika maeneo yaliyo karibu na mahali walikotoka wakati wa zahma hiyo. Kwa mujibu swa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR zoezi hilo linaendeshwa kwa ushirikiano na serikali ya Msumbiji na washirika wengine .