Silaha za kemikali zimetumika Douma au la?
Uchunguzi umeanza kuweza kubaini iwapo silaha za kemikali zimetumika kwenye shambulio dhidi ya raia huko Douma, nchini Syria.
Uchunguzi umeanza kuweza kubaini iwapo silaha za kemikali zimetumika kwenye shambulio dhidi ya raia huko Douma, nchini Syria.
Iwapo Baraza la Usalama halitatumia mamlaka yake ya kuleta amani Syria nani ataweza kufanya hivyo?
Ni moja ya kauli lukuki zilizotamalaki wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichokutana leo kutathmini utekelezaji wa azimio lake namba 2401 la kutaka sitisho la mapigano nchini Syria.
Zaidi ya mwezi mmoja tangu kupitishwa kwa azimio hilo bado hali ya usalama na kibinadamu si shwari.
Umoja wa Mataifa na wadau wake wanakumbwa na mkwamo siyo tu kwenye kuwasilisha misaada ya kibinadamu, bali pia kuwahamisha wagonjwa mahututi.
Syria! Syria! Syria! Bado ni kizungumkuzi, maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanapitishwa lakini wahusika ni kama kusema "wameweka pamba masikioni."
Choo kimoja kutumiwa na watu 200, gharama ya yai moja ni dola 4, mfuko mmoja wa mkate dola 4, ni simulizi kutoka kwa wakimbizi walioweza kukimbia kutoka eneo la Ghouta Mashariki nchini Syria.
Ni katika eneo hilo ambako makombora yanaendelea kuporomoshwa mfululizo licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka sitisho la mapigano ili huduma ziwafikie walengwa.
Mwaka wa 7 wa mzozo wa Syria umekamilika na sasa mwaka wa 8 umeanza na hakuna nuru ya kumalizika kwa mzozo huo, lakini bado tusikate tamaa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo.
Akifungua kikao cha 37 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi hii leo, Bwana Guterres amesema ingawa tamko la haki za binadamu mwaka huu linatimiza miaka 70 bado haki hizo zinapuuzwa.
(Sauti ya Antonio Guterres)
Mapigano huko Ghouta Mashariki nchini Syria yakiendelea kugharimu maisha ya watu, hii leo wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamepatiwa nukuu za mashuhuda ya athari za makombora yanayoendelea kuporomoshwa kwenye eneo hilo kwa mfululizo tangu tarehe 4 mwezi huu.
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, Mark Lowcock amesoma nukuu hizo zilizowasilishwa kwao na wafanyakazi wa kutoa misaada nchini Syria.
Katika nukuu hii Bwana Lowcock anasema kuna familia nzima inalengwa. Mama na watoto wake watatu. Wanawake wajawazito wanne.
Syria hali inazidi kuwa mbaya zaidi , raia wanakabiliwa na mashambulizi. Tangu tarehe 4 mwezi huu wa Februari raia zaidi ya 300 wameuawa kwenye mapigano kati ya serikali na wapinzani.
Mzozo wa Syria sasa ukielekea mwaka wa nane, bado mapigano yanazidi kushika kasi, watoto wakiwa hatarini zaidi na haki zao za msingi zikisiginwa na watu wazima wasiojali chochote.