General Assembly

Hapa na pale (Taarifa za kusoma)

Kikao cha 63 Baraza Kuu la UM kiliongozwa na Raisi wa mwaka huu Miguel d’Escoto Brockmann wa Nicaragua. Kabla ya Raisi wa Baraza Kuu kufungua rasmi majadiliano ya wawakilishi wote, KM wa UM Ban Ki-moon alihutubia kikao kwenye ukumbi wa Baraza Kuu ambapo aliwasilisha taarifa ya mapitio ya mwaka kuhusu shughuli za UM ulimwenguni. Baada ya hapo Raisi Miguel d’Escoto alihutubia wawakilishi wa Mataifa Wanachama 192, na alifuatiwa na Raisi Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil ambaye taifa lake, kwa kulingana na mila za UM, huwa ni taifa la awali kuongoza majadiliano ya jumla kwenye Baraza Kuu.

Viongozi wa dunia watathminia maendeleo Afrika

Baraza Kuu la UM leo hii limeanzisha mkutano maalumu wa watu wa ngazi za juu, kuzingatia, kwa sikui nzima, mahitaji ya maendeleo kwa bara la Afrika, kwa sababu ya wasiwasi uliojiri wenye kuonyesha bara la Afrika lipo nyuma sana, tukilinganisha na maeneo mengine, katika kutekeleza ile kampeni ya kimataifa ya kupunguza kwa nusu, katika 2015, hali ya ufukara, kutojua kusoma na kuandika na maradhi mengineyo ya kijamii.

Baraza la Usalama linazingatia Chad na JAK

Baraza la Usalama Ijumaa limezingatia ripoti ya karibuni ya KM juu ya hali ya usalama katika Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK). Ndani ya ripoti KM amependekeza UM upeleke vikosi vya kulinda amani vya UM vya wanajeshi 6,000 wanaotakikana kuchukua nafasi ya vikosi vya Umoja wa Ulaya viliopo Chad mashariki na kaskazini-mashariki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, maeneo ambayo katika miaka ya karibuni yaliharibiwa na fujo na vuruguu, na kusababisha halaiki ya raia kungo’lewa makazi na kuelekea kwenye maeneo mengine walipopatiwa uhamisho wa muda.~

Raisi mpya wa BK ahimiza demokrasia ihuishwe katika UM

Raisi mpya wa Baraza Kuu la UM, Miguel D’Escoto Brockmann, aliyekuwa Waziri wa Nchi za Nje wa Nicaragua, jana jioni alifungua rasmi kwenye Makao Makuu ya UM kikao cha 63 kinachojumuisha Mataifa Wanachama 192 kutoka kila pembe ya dunia, ambapo wajumbe wao hukusanyika kila mwaka, kuanzia mwezi Septemba hadi Disemba, kuzingatia masuala yote muhimu ya kimataifa, na kuchukua maamuzi kwa kulingana na kanuni za Mkataba wa UM.

Baraza Kuu linazingatia pendekezo la kupiga vita ugaidi duniani

Baraza Kuu la UM limekutana wiki hii kwa siku mbili, kwenye kikao cha wawakilishi wote kuzingatia azimio la kupiga vita ugaidi duniani. Kulifanyika majadiliano maalumu yaliofanya mapitio juu ya lile azimio la 2006 la Kuratibu Mipango ya Pamoja Kupiga Vita Ugaidi Ulimwenguni.

Hapa na pale

Kikundi Kazi cha Baraza Kuu kinachosimamia juhudi za kukomesha na kufyeka ukandamizaji wa kijinsia, na unyayanyasaji miongoni mwa watumishi wa UM, wamepitisha azimio muhimu karibuni litakalowahakikishia waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia kuwa wanapatiwa tiba maridhawa, ushauri, misaada ya jamii na vile vile msaada wa kisheria.

Mjadala wa wawakilishi wote kuhitimishwa kwenye Baraza Kuu la UM

Mjadala wa wiki mbili wa wawakilishi wote kwenye Baraza Kuu la UM ulihitimishwa hapo Ijumatano kwa moyo mzito. Mjadala huu, wa kikao cha 61 cha Baraza Kuu, ulihudhuriwa na maofisa mbalimbali, wa vyeo vya juu, kutoka Serekali wanachama, maofisa ambao wingi wao walihimizana kuongezwe uangalifu wa jumla miongoni Mataifa Wanachama, ili kuhifadhi heshima na hadhi ya UM katika kazi zake.

Mukhtasari unaongaza wiki ya kwanza ya mjadala wa wawakilishi wote katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Mjadala wa kila mwaka wa wawakilishi wote kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulifunguliwa rasmi hapo Ijumanne, tarehe 19 Septemba (2006) na Sheikha Haya Rashed Al Khalifa wa Bahrain. Sheikha Haya katika hotuba yake ya ufunguzi aliwahimiza viongozi wa kimataifa waliokusanyika kwenye Makao Makuu kulenga zaidi juhudi zao katika kutekeleza kwa vitendo ahadi zao ili kusaidia kupunguza ufukara na kuboresha maisha ya umma wa kimataifa, kwa ujumla. ~

Kumbukumbu ya ziara ya Makamu KM juu ya Masuala ya Kiutu katika Afrika

Mapema wiki hii Jan Egeland, Makamu KM Juu ya Misaada ya Kiutu ya Dharura alikutana na waandishi habari mjini Nairobi, Kenya baada ya kukhitimisha safari ya siku nane kwenye maeneo matatu yaliokabiliwa na matatizo ya kiutu barani Afrika; yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (JKK), Uganda na Sudan ya Kusini.