General Assembly

Hapa na Pale (Taarifa za Kusoma)

UM umeripoti kwamba yale mashirika yanayohudumia misaada ya kihali yameamua kukuza mchango wa dharura katika Usomali ili kuwanusuru maisha watu 15,000 waliong’olewa makazi karibuni katika mji wa Mogadishu, kwa sababu ya mapigano makali yaliofumka kwenye eneo hilo. Inaripotiwa raia 80 waliuawa na mamia wengine walijeruhiwa kwenye uhasama amabo makali yake hayajawahi kushuhudiwa nchini kwa muda wa zaidi ya mwaka na nusu.

Raisi wa Tanzania azingatia umuhimu wa Malengo ya Milenia kukuza maendeleo Afrika

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, kwenye taarifa alioitoa mbele ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Baraza Kuu (BK) juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), alitilia mkazo “umuhimu mkubwa mno” wa mkusanyiko wao. Alikumbusha ya kwamba mnamo tarehe 22 Septemba KM aliitisha mkutano wa ngazi ya juu kuzingatia mahitaji ya kukuza huduma za maendeleo katika bara la Afrika.

Mapitio ya siku ya pili ya majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu

Waziri Mkuu wa Uchina Wen Jiabao aliwaamabia wajumbe waliohudhuria kikao cha wawakilishi wote cha Baraza Kuu kwamba sera adhimu ya taifa lake ni kufuatilia njia ya amani kukuza maendeleo,wakati ikijenga nguvu za kijeshi kwa makusudio pekee ya kulinda na kuhami uhuru wake na umoja wa nchi. Alisema Uchina hauna dhamira yeyote ya “kumiliki dunia, si sasa wala si katika siku zijazo.”

Hapa na Pale (Taarifa za Kusoma)

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba wiki iliopita watu 12,000 waliuhajiri mji wa Mogadishu, Usomali kwa sababu ya mapigano makali yaliozuka baina ya wapiganaji wafuasi wa makundi ya KiIslam, wenye kupinga serikali, dhidi ya na vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia yaliopo nchini. Nusu ya wahamiaji waliong’olewa makwao walipatiwa makazi ya muda karibu na mji, na nusu nyengine walikimbilia mji wa Afgooye ,uliopo kilomita 3o kusini-magharibi ya Mogadishu.

Mukhtasari wa siku ya pili ya majadiliano ya jumla katika Baraza Kuu

Waziri Mkuu wa Uchina Wen Jiabao aliwaambia wajumbe waliohudhuria kikao cha wawakilishi wote cha Baraza Kuu kwamba sera adhimu ya taifa lake ni kufuatilia njia ya amani kukuza maendeleo,wakati ikijenga nguvu za kijeshi kwa makusudio pekee ya kulinda na kuhami uhuru wake na umoja wa nchi. Alisema Uchina hauna dhamira yeyote ya “kumiliki dunia, si sasa wala si katika siku zijazo.” Alifahamisha kwamba nchi yake haitishii taifa lolote, na kusisitiza Uchina inajivunia pakubwa kwa mafanikio yake katika ustawi wa kiuchumi, kuendeleza haki ya jamii, upole wa raia zake na uadilifu wenye nguvu.~

Raisi wa Kenya asema taifa limepiga hatua muhimu baada ya vurugu

Majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu (BK) la UM, kwenye kikao cha wawakilishi wote, yaliendelea mnamo alasiri ya siku ya mwanzo ya mahojiano ambapo Raisi Mwai Kibaki wa Jamhuri ya Kenya, alipohutubia mkutano, alisema nchi yake imepiga hatua muhimu kwenye maafikiano ya kurekibisha sheria, katiba na masuala mengine yanayaohitajika kutekelezwa ili kuepukana na na hatari ya kurudia tena vurugu kama lile liliozuka nchini mwanzo wa mwaka baada ya uchaguzi.

Wakulima wadogo wadogo wanazingatiwa misaada ya kujitegemea

Hapa Makao Makuu leo asubuhi kulifanyika warsha kadha wa kadha juu ya masuala yanayohusu juhudi za kukuza maendeleo katika nchi maskini. Kwenye mkusanyiko mmoja kuliwasilishwa mradi mpya utakaofadhiliwa na wakf za kimataifa na kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kukuza pato na kujitegemea kimaisha.

Hapa na pale (Taarifa za kusoma)

Ripoti iliotayarsihwa bia na Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO), Shirika la Hifadhi ya Mazingira (UNEP), Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi wa Kimataifa na vile vile Shirika la Kimataifa la Waajiri inaashiria shughuli za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa zikitekelezwa zina uwezo wa kuzalisha mamilioni ya fursa za ajira mpya itakayozozalisha “uchumi wa ajira ya kijani.” Mradi huu unatarajiwa kusaidia zile juhudi za kupunguza hewa chafu inayomwagwa angani yenye kuharibu mazingira, inayotokana na matumizi ya nishati ya petroli. Ripoti ilipewa jina la “Vibarua vya Kijani: Kuelekea Kwenye Kazi Stahifu Katika Ulimwengu Unaosarifika wenye Kaboni ya Chini.”

Kikao cha 63 cha Baraza Kuu la UM chafunguliwa rasmi

Majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu la UM, kwenye kikao cha wawakilishi wote yalianzishwa rasmi asubuhi ya leo ambapo viongozi wa kimataifa waliwasilisha hoja zao kadha wa kadha kuhusu utaratibu unaofaa kuzingatiwa kimataifa ili kukabiliana na matatizo ya ulimwengu kipamoja.

Rais wa Baraza Kuu ahimiza ushikamanao kukabili matatizo ya ulimwengu

Rais wa Baraza Kuu la UM, Miguel d’Escoto Brockmann alipofungua majadiliano ya jumla ya kikao cha mwaka huu cha 63 cha UM, aliwaambia wawakilishi wa Mataifa Wanachama 192 ya kwamba wakati umewadia kwa umma wa kimataifa “kuchagua njia iliyoongoka ya ushikamano na umoja” kukomesha kile alichokiita utamaduni wa uchoyo na ubinafsi, ustaarabu, ambao alisihi husababisha mamilioni ya umma wa ulimwengu kusumbuliwa na umaskini pamoja na matatizo mengineyo yalizushwa na wanadamu wenyewe.