General Assembly

Kumbukumbu za mikutano kwenye Baraza Kuu

Ijumatatu, Baraza Kuu la UM linajadilia ripoti ya Baraza la Maendeleo ya Uchumi na Jamii (ECOSOC); na pia kuzingatia masuala juu ya uhusiano wamashirika ya kikanda na mengineyo na UM. Kadhalika wajumbe wa kimataifa wanafanya mapitio kuhusu ripoti ya KM ya kumbukumbu za majanga ya maangamizi ya halaiki, hususan lile janga la maangamizi ya wafuasi wa dini ya Kiyahudi kwenye Vita Kuu ya Pili. ~

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania atathminia kikao cha 63 cha Baraza Kuu la UM

Taarifa ya wiki hii inazingatia tathmini ya Waziri wa Mambo ya ~na Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bernard Membe, juu ya kikao cha 63 cha Baraza Kuu la UM. ~~

Mjadala wa mwaka wa BK umemalizika na Raisi wake ahamasisha mabadiliko ya kidemokrasia katika UM

Kwa muda wa karibu wiki mbili hivi, Wakuu wa Taifa na Serikali 111 walisimama mbele ya wajumbe wa kimataifa, kwenye ukumbi wa Baraza Kuu kuelezea wasiwasi walionao juu ya masuala kadha muhimu ambayo wangelipendelea kuona yanapewa usikivu mzuri zaidi na jumuiya ya kimataifa.

Kamati ya Kwanza ya BK imepitisha ajenda ya kikao cha 63

Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu (BK), inayohusika na Masuala ya Usalama wa Kimataifa na Upunguzaji wa Silaha imepitisha ajenda na ratiba ya kikazi kuzingatiwa kwenye kikao cha safari hii cha 63, ikijumlisha suala la kuzuia mashindano ya silaha nje ya dunia, na kukomesha biashara haramu ya silaha ndogo ndogo na nyepesi, pamoja na suala la kujikinga na hatari ya magaidi kupata silaha za maangamizi ya halaiki.~

Hapa na Pale

Zhang Yesui Mjumbe wa Kudumu wa Uchina katika UM atachukua uongozi wa Uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba, baada ya Michel Kafando, Mjumbe wa Kudumu wa Burkina Faso kumaliza muda wa Mwenyekiti wa Baraza kwa mwezi Septemba.

Syria imeambia UM mazungumzo na Israel yana matumaini ya amani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid Al-Moualem leo Ijumamosi aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliohudhuria kikao cha Baraza Kuu cha wawakilishi wote ya kwamba mazungmzo yasiodhahiri yanayofanyika sasa na Israel, yanayoongozwana Uturuki, yana uwezo wa kuandaa amani kati yao pindi vipengele fulani vitakamilishwa.

Mizozo ya kimataifa karne ya sasa yahitajia suluhu za washiriki wingi, inasisitiza Ujerumani

Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeir Ijumaa alilwaambia wajumbe waliohudhuria kikao cha 63 cha Baraza Kuu hapa Makao Makuu ya kwamba matatizo muhimu yanayokabili ulimwengu wetu kwa sasa hayatoweza kupatiwa suluhu ya kuridhisha mpaka pale nchi zote za ulimwengu zitakapochangisha juhudi zao kipamoja kuyatatua masuala hayo – kuanzia masuala ya kurudisha utulivu katika Afghanistan na Pakistan, kuimarisha amani Mashariki ya Kati na kupunguza urimbikizaji na pia matumizi ya silaha za mauaji ya halaiki ulimwenguni.

Hapa na Pale

Baraza la Usalama limepitisha, kwa kauli moja, azimio linaloitaka Iran kutekeleza, haraka, kwa ukamilifu yale maazimio yaliopita ya Baraza yalioshurutisha kusitishwa shughuli za kusafisha madini ya yuraniamu halisi inayotumiwa ama kuzalisha nishati ya umeme au silaha, na kuitaka ishirikiane nawakguzi wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA). ~~

Katibu Mkuu apongeza mafanikio ya kikao maalumu cha MDGS

Baada ya mikutano ya ngazi za juu pamoja na warsha kadha wa kadha zilizofanyika siku nzima hapa Makao Makuu, Alkhamisi ya jana, kupitia namna utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) unavyoendelezwa, wajumbe waliowakilisha serikali, taasisi za kimataifa, jumuiya za kiraia na mashirika ya wafanyabiashara waliungana kipamoja na kuitika mwito wa kuchukua hatua za utendaji wa dhahrura ili kupunguza, kwa kima kikubwa, itakapofika 2015, janga la ufukara, njaa iliokithiri, magonjwa yanayozuilika na maafa mengine ya kiuchumi na jamii yenye kusumbua umma wa nchi zinzoendelea.

Baraza la Usalama lakutana kuzingatia Mashariki ya Kati

Baraza la Usalama hii leo limekutana kuzingatia suala la Mashariki ya Kati, ikijumuisha tatizo la makazi ya walowezi wa Israel kwenye maeneo ya Wafalastina. ~ ~