General Assembly

Baraza Kuu lafanikiwa kupitisha bajeti la 2010-2011 kwa shughuli za UM

Alkhamisi iliopita, Baraza Kuu la UM lilifanikiwa kupitisha bajeti la UM kwa miaka miwili ijayo, miaka ya 2010-2011, bajeti ambalo linagharamiwa dola bilioni 5.16.

Rais wa BK asema karidhika na shughuli za kikao cha 2009

Ali Abdussalam Treki wa Libya, Raisi wa kikao cha 2009 cha Baraza Kuu (BK) la UM - kikao cha 64 - Ijumanne adhuhuri, alikuwa na mahojiano ya kufunga mwaka, na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu.

Baraza Kuu laitisha Mkutano Mkuu mwakani kuharakisha utekelezaji wa MDGs

Baraza Kuu la UM limepitisha azimio la kuitisha, katika mwezi Septemba mwakani, mkutano mkuu, utakaohudhuriwa na wawakilishi wote wa kimataifa, kwa madhumuni ya kusailia maendeleo kwenye utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Raisi wa BK anatabiri 'enzi mpya ya uhusiano wa kimataifa' wakati wa kufunga majadiliano ya wawakilishi wote

Ijumanne mchana Baraza Kuu la UM lilikamilisha wiki moja ya majadiliano ya mwaka ya wawakilishi wote, ambapo wajumbe kutoka nchi 192 walizungumza, ikijumlisha Wakuu wa Mataifa na Serikali 107, waliowasilisha hoja kadha juu ya sera za kuendeleza uhusiano wa kimataifa.

KM ameridhika na mahojiano ya awali kwenye kikao cha mwaka cha BK

KM Ban Ki-moon alifanya mahojianio na waandishi habari kwenye Makao Makuu ya UM, leo asubuhi, na aliwaambia wanahabari kwamba maendeleo makubwa yalipatikana tangu kikao cha 64 cha Baraza Kuu (BK) kuanza rasmi wiki iliopita, ambapo viongozi wa dunia walifikia maafikiano kadha kwenye juhudi zao za kutafuta suluhu ya kuridhisha ya masuala makuu yanayotatanisha ulimwengu wetu, ikijumlisha udhibiti wa madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, ukomeshaji wa silaha za maangamizi za kinyuklia na kwenye mizozo ya kifedha katika soko la kimataifa.

Namibia kuyasihi Mataifa Wanachama kupitisha hatua kali dhidi ya serikali zinazochukua madaraka kimabavu

Majadiliano ya wawakilishi wote bado yanaendelea kwenye ukumbi wa Baraza Kuu na yameingia siku ya sita hii leo.

Baraza Kuu laanzisha tena majadiliano ya jumla ya mataifa wanachama

Majadiliano ya jumla kwenye kikao cha mwaka cha wawakilishi wote, yameanza tena rasmi leo asubuhi hapa kwenye Makao Makuu, kufuatia kikao cha siku nzima cha Baraza Kuu kilichokusanyika Ijumamosi, ambapo wazungumzaji waliowakilisha mataifa 30 waliwakilisha hoja kadha wa kadha kuhusu taratibu wa kusuluhisha masuala yenye kusumbua umma wa kimataifa.

Mataifa Wanachama yalioshiriki kwenye majadiliano ya mwaka kudai mageuzi ya kidemokrasia katika shughuli za UM

Majadiliano ya jumla ya mwaka kwenye kikao cha 64 cha Baraza Kuu la UM leo yameingia siku ya tatu.

Majadiliano ya wawakilishi wote kwenye Baraza Kuu yameingia siku ya pili

Majadiliano ya jumla, kwenye kikao cha wawakilishi wote katika Baraza Kuu la UM, leo yameingia siku ya pili.

Suluhu ya wahusika wengi ndio inayohitajika kutatua mizozo ya kimataifa, asihi Raisi wa BK

Raisi wa Baraza Kuu (BK), Ali Treiki wa Libya, kwenye risala yake ya ufunguzi wa majadiliano ya jumla, aliyahimiza Mataifa Wanachama kushirikiana, kwa ukaribu zaidi, na taasisi ya UM.