GAZA

Hali katika Gaza ni tete, pande zote sitisheni ghasia: Mladenov

Ghasia katika maeneo yanayokaliwa kwa nguvu na Israel kwenye ukingo wa magharibi wa mto Jordan ikiwemo Yerusalem Mashariki zinaongezeka huku mamlaka ya Israel ikiendelea na bomoabomoa na kuchukua kwa nguvu  nyumba za wapalestina.

Hatutakubali tena upatanishi wa Marekani pekee- Rais Abbas

Wapalestina pamoja na eneo lao hivi sasa wanahitaji zaidi ulinzi wa haraka kutoka kwa jamii ya  kimataifa kuliko wakati wowote ule.

Kuongezeka kwa ukatili Gaza kunatishia kuzuka kwa vita- DiCarlo

Mkuu wa masuala ya siasa kwenye Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo ameliambia Baraza la Usalama la umoja huo kuwa kuongezeka kwa ghasia kunatishia vita Gaza na kwamba msaada wa kibinadamu kwa ajili ya ukanda huo haupaswi kuzuiliwa kwa kuangalia mabadiliko ya kisiasa na kiusalama.

UNRWA  yapata fedha lakini zatosha mwezi mmoja tu

Baada ya vuta nikuvute na kutokuwa na uhakika wa ufadhili kwa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada kwa wakimbizi wa kipalestina UNRWA, hatimaye kuna matumaini baada ya baadhi ya wahisani kujitokeza kusaidia angalau shule ziweze kufunguliwa mwezi ujao.

Ahsante EU kwa msaada wako kwa watu wa Gaza- WFP

Muungano wa Ulaya EU umelipatia shirika la mpango wa chakula duniani, WFP zaidi ya dola milioni 3 kwa ajili ya kusaidia kununua chakula cha wapalestina walioko ukanda wa Gaza  huko Mashariki ya Kati.

Dola milioni 17 kukwamua vijana Ukanda wa Gaza

Benki ya Dunia imetangaza mkopo nafuu wa dola milioni 17 kwa ajili ya mradi wa kusaidia vijana wasio na ajira huko ukanda wa Gaza Mashariki ya kati kujipatia kipato na kuweza kuajirika.

Kuzuia kuingia mafuta Gaza ni hatari inayoweka rehani maisha ya mamilioni ya wagonjwa:McGoldrick

Vikwazo dhidi ya kuingiza mafuta ya dharura yanayohitajika haraka Gaza, ni kitendo cha hatari ambacho kina athiri kubwa kwa haki za watu wa Gaza na kuyaweka rehani maisha yao.

Tume ya kuchunguza yaliyojiri katika maandamano ya Gaza 2018 yateuliwa:UN

Watu watatu wameteuliwa na baraza  la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa katika jopo maalum litakalochunguza  yaliyojiri katika maandamano ya mwaka 2018 kwenye maeneo yanayokaliwa ya Palestina.

Wapalestina wateseka

 Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein amesema   kumekuwa na uchunguzi mdogo sana dhidi ya vikosi vya ulinzi vya Israel ambavyo vinatekeleza ukatili dhidi ya Wapalestina na hata unapofanyika huna nguvu dhidi ya washutumiwa kuweza  kuchukuliwa hatua za kinidh

Sauti -
2'44"

Utaratibu wa Israel unaenda kinyume na sheria za haki za kimataifa:Zeid

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein amesema   kumekuwa na uchunguzi mdogo sana dhidi ya vikosi vya ulinzi vya Israel ambavyo vinatekeleza ukatili dhidi ya Wapalestina na hata unapofanyika hauna nguvu dhidi ya washutumiwa kuweza  kuchukuliwa hatua za kinidhamu na hukumu ikitolewa  huwa ni ndogo ikilinganishwa na makosa yaliyofanywa.