Kujiondoa kwa Mali kwenye G5 Sahel na Jeshi la Pamoja ni 'kizuizi' kwa eneo hilo
Uamuzi wa nchi ya Mali mnamo Mei 15 kujiondoa katika kundi la G5-Sahel na Jeshi lake la Pamoja ni "bahati mbaya" na "wa kusikitisha", Martha Ama Akyaa Pobee ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Afrika, katika idara ya masuala ya Siasa, ujenzi wa amani na kulinda amani jana Jumatano ameliambia Baraza la Usalama, huku akizitaka nchi za eneo hilo kuongeza juhudi za kulinda haki za binadamu, huku kukiwa na migogoro ya muda mrefu ya kisiasa na kiusalama.