G-start

Vijana Nyeri Kenya waona nuru ya maisha kupitia usindikaji wa ndizi 

Chukua vijana wajasiriamali, wapatie vifaa vya kisasa na mafunzo basi utakuwa umebadilisha maisha si ya kwao tu bali na jamii zao ,na hicho ndio kilichotokea huko kaunti ya Nyeri nchini Kenya baada ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya kushikana mikono na kunasua vijana ambao walikuwa kidoto wakate tamaa.