13 JANUARI 2022
Miongoni mwa tuliyonayo hii leo katika habari za Umoja wa Mataifa
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO linasema kuwa japokuwa habari mbayá ni kuwa Omicron ambao ni mnyumbuliko wa virusi vya corona ulichochea wimbi la nne la Covid-19 barani Afrika lakini unapungua haraka kuliko mawimbi yaliyotangulia kama lile la mnyumbuliko aina ya Delta. Hata hivyo idadi ya waliopata chanjo dhidi ya Covid-19 barani humo baado ni ndogo mno.