Kuna ongezeko la hatari dhidi ya watoto CAR - UNICEF
Mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, NCHINI Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Fran Equiza, hii leo akizungumza na wanahabari mjini Geneva Uswisi amesema, "watoto 370,000 kwa sasa ni wakimbizi wa ndani nchini kote kwa sababu ya vurugu zinazoendelea na ukosefu wa usalama. Hiki ni kiwango cha juu kabisa cha watoto kufurushwa katika makazi yao tangu 2014."